×

Miradi ya NHC Yaibua Hamasa; Zanzibar, GPR Na Kawe 711 Kuwa Darasa La Makazi Ya Kisasa

Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Zanzibar, Mhe. Rahma Kassim Ally, akiongozana na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Miundombinu, Ardhi na TEHAMA ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar pamoja na viongozi wa Shirika la Nyumba la Zanzibar (ZHC), ametembelea miradi ya Golden Premier Residence (GPR) na Kawe 711 inayotekelezwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) jijini Dar es Salaam.

Ziara hiyo imelenga kujifunza na kubadilishana uzoefu kuhusu usanifu, teknolojia za kisasa, viwango vya ujenzi na usimamizi wa miradi ya makazi.

Katika ziara hiyo, ujumbe ulipata fursa ya kujionea maendeleo ya miradi hiyo, kutembelea nyumba za mfano na kupata maelezo kuhusu mikakati ya NHC katika kuendeleza makazi ya kisasa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa ZHC, Bw. Sultani Saidi Suleimani, amesema miradi ya NHC imekuwa darasa muhimu kwa taasisi yao na kwamba uzoefu walioupata utasaidia kuboresha utekelezaji wa miradi ya nyumba Zanzibar.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Bw. Hamad Abdallah, amesema Shirika litaendelea kuimarisha ushirikiano na ZHC kupitia kubadilishana maarifa na uzoefu, ikiwemo kufanya ziara Zanzibar kujionea miradi inayotekelezwa na taasisi hiyo.

Leave a Comment