×

Davido Ajizawadia Gari la Kifahari la Brabus Lenye Thamani ya Tsh Bilioni 5.6 Kutimiza Miaka 34

STAA mkubwa wa muziki wa Afrobeats kutoka Nigeria, David Adeleke maarufu kama Davido, anaripotiwa kujizawadia gari la kifahari aina ya Customized Mercedes-Benz BRABUS XLP 800 G-Wagon ikiwa ni sehemu ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa ya kutimiza miaka 34.

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa na The Buzz Central kupitia mwandishi Kacy Lee, Novemba 24, 2026, Davido ametumia kiasi kinachodaiwa kuwa ni dola za Marekani milioni 2.1, sawa na takribani TSh bilioni 5.6, kununua gari hilo lenye muonekano wa kipekee wa rangi ya zambarau.

Msanii huyo anaripotiwa kuonekana akichukua gari hilo la kifahari, ambalo tayari limevutia hisia za mashabiki pamoja na wapenda magari ya kifahari.

BRABUS XLP 800 ni gari lenye teknolojia na uwezo mkubwa, likiwa na injini ya V8 Twin-Turbo yenye uwezo wa kuzalisha nguvu za farasi 800 (800 HP) na torque ya 1,000 Nm. Pia lina muundo maalumu wa pickup unaolifanya kuwa tofauti na G-Wagon za kawaida.

Leave a Comment