×

Zuchu Aanika Zawadi ya Mkoba wa Dior Aliyopewa Na Diamond

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Zuchu, ameonyesha furaha yake kupitia mtandao wa Snapchat baada ya kupokea zawadi ya mkoba wa kifahari kutoka kwa mwanamuziki Diamond Platnumz.

Zuchu ameshare picha ya mkoba huo wenye nembo ya kampuni maarufu ya mitindo ya Dior, huku akimshukuru Diamond kwa zawadi hiyo na kumuombea baraka zaidi katika riziki yake.

Kupitia ujumbe aliouandika kwenye picha hiyo, Zuchu ameonekana kumshukuru kwa kile alichokitoa, akimuombea Mwenyezi Mungu amrejeshee zaidi ya alichotumia.

“Thank you ba mtu, Allah akurejeshee pakubwa ulipotoa, akuongezee riziki, usikaikiwe. Amina,” ameandika Zuchu.

Zawadi hiyo imeibua hisia za furaha kwa Zuchu, ambaye ameamua kushirikisha wafuasi wake kwenye mtandao huo picha ya mkoba huo wa kifahari.

Leave a Comment