The House of Favourite Newspapers

GOLDEN STATE WANACHAPA TU, SASA NI 2-0

WABISHI Golden State Warriors juzi walifanya maajabu tena baada ya kuwachapa Cleveland Cavaliers kwenye mchezo wa pili wa fainali ya NBA.

Staa Stephen Curry, aliendelea kuonyesha umwamba wake kwenye mchezo huo na sasa wanaongoza kwa 2-0 ikiwa imebaki michezo mitano kati ya saba ya fainali wanayotakiwa kucheza.

Curry aliiongoza timu yake kupata  122-103, katika mchezo mkali ulipopigwa kwenye Dimba la Oracle Arena.

 

Curry ambaye amekuwa akipambana na staa LeBron James, kwenye ubora wa NBA aliiongoza timu yake kwa kufunga pointi 33 kwenye mchezo huo ukiwa ni ushindi wao wa pili mfululizo na wanapewa nafasi kubwa ya kutetea ubingwa wao.

“Huu ni usiku mzuri sana, nafikiri kuwa mambo yataendelea kuwa mazuri siku zijazo, kwa sasa tayari tumeshinda michezo miwili jambo ambalo ni zuri sana kwetu,” alisema Curry.

Kevin Durant, aliendelea kuonyesha umwamba wake baada ya kufunga pointi 26 kwenye mchezo huo akiwa ana rebaundi tisa na asisti saba.

 

Klay Thompson, yeye alifunga pointi 20 kwenye mchezo ambao alionyesha uwezo wa juu uwanjani.

James ambaye mchezo wa kwanza aliongoza kwa kufunga pointi 51, juzi alipunguza kasi yake baada ya kufunga pointi 29 tu, staa huyo alitupia pia pasi 13 na rebaundi tisa lakini bado timu yake ilipata kichapo.

”Lazima tuendelea kuishi bila furaha, hata kama tunakwenda kucheza nyumbani haimaanishi kuwa tunatakiwa kuona mambo yatakwenda vizuri, siyo kweli,” alisema James.

Kevin Love, ambaye hajawa na msimu mzuri alifanikiwa kufunga pointi 22 kwenye mchezo huo jambo ambalo lilionekana pia kutomfurahisha.

Bado mashabiki waamini kuwa mchezo wa tatu wa ligi hiyo Curry na James ndiyo wanaweza kufanya maamuzi ambao utapigwa kesho kwenye Dimba la Quicken Loans Arena.

 

“Tutakwenda kupambana, hakuna kinachozuia mapambano kama bado hujafanikiwa unachokitaka, nafikiri tunaweza kufanya vizuri sana kama tutaendelea kuwa na umoja huu, hiki ni kitu pekee ambacho kinaweza kutupa ubingwa huu mwaka huu,” alisema tena Curry.

 

JaVale McGee alifanikiwa kufunga pointi 12, kwenye mchezo huo ukiwa ni mchezo wake wa kwanza anaanza kwenye ligi ya NBA msimu huu.

 

Kama Warriors wakiweza kushinda mchezo mmoja kati ya miwili ambayo itapigwa ugenini Juni 7 na 9, basi watakuwa na uhakika wa asilimia kubwa wa kutwaa ubingwa huo kwa mara ya pili.

Msimu uliopita walitwaa ubingwa huo bila jasho na inaonekana kuwa wanaweza tena kutwaa ubingwa wa mwaka huu kwa staili hiyo hiyo.

 

Kocha Steven Kerr, amekuwa kwenye kiwango cha juu na ameiongoza timu hiyo kuwa na wachezaji wengi mahiri hali ambayo inampa nafasi kubwa ya kuwa kocha bora wa ligi hiyo msimu huu.

Golden State wamekuwa wakishinda kwa kuwa wana wachezaji wengi mahiri, tofauti na Claveland Cavalliers ambao wamekuwa na wachezaji wachache sana wanaoweza kubadilisha matokeo.

GAME 1: Golden Warriors Waichapa Cleveland Cavaliers 124-114

Comments are closed.