MWIMBAJI wa kundi la Little Mix, mrembo Perrie Edwards, anamwinda mcheza soka wa timu ya England na Arsenal, Alex Oxlade-Chamberlain.
Mdada huyo mwenye umri wa miaka 23 alikuwepo katika mtanange wa Ligi Kuu ya Uingereza wakati Arsenal ilipokutana na Tottenham Hotspurs ili kumwona mwanasoka huyo ambaye walianza mahusiano ya siri hapo nyuma. Katika mechi hiyo timu hizo zilitoka sare ya 1-1.
Perri amejikita katika penzi hilo baada ya kuachana na mwimbaji wa kundi la One Direction aitwaye Zayn Malik na nyota mwingine wa kunid la Our Girl, Luke Pasqualino, ambaye alionekana akibadilishana naye mabusu ya nguvu mwezi uliopita.
Alex aliichezea England michezo 24 na kushiriki katika mchezo wa sare ya 2-2 kati ya Arsenal na Paris St Germain katika Ligi ya Mabingwa iliyochezwa juzi.
Perrie akiwa na Luke Pasqualino
Hata hivyo, habari zinasemekana kwamba Alex ameeleza nguvu zake katika soka ili aweze kupata namba ya kudumu katika timu yake ya Arsenal.
Sanchoka Amponza Idriss, Amwagwa

