×

Timu iliyopata ajali Brazil yatakiwa kucheza mechi

rescuers-search-for-survivors-from-the-wSANTOS, Brazil

LICHA ya kupoteza wachezaji wengi katika ajali ya ndege iliyotokea wiki hii, timu ya Chapecoense inaweza kulaz­imika kuingia uwanjani kucheza mchezo wa Ligi Kuu ya Brazil ‘Serie A’ kama kawaida wikiendi ya wiki ijayo.

Chapecoense ilipoteza idadi kubwa ya wachezaji kutokana na ajali hiyo ilipokuwa njiani ikielea Co­lombia kucheza fainali ya Copa Suda­mericana dhidi ya Atletico Nacional.

Makamu wa rais wa zamani klabu­ni hapo, Ivan Tozzo ambaye ame­kuwa akifanya shughuli nyingi za klabu hivi karibuni amesema Rais wa Chama cha Soka cha Brazil, Marco Polo del Nero amewataka wacheze Desemba 11, dhidi ya Atletico Mi­neiro.

“Aliniambia juu ya suala hilo nikamjibu kuwa mpaka sasa hatuna kikosi cha kwanza, akaniambia ‘nyie mnao wachezaji, si wapo vijana wa chini ya miaka 20, wapo pia ambao walikuwa majeruhi kama watano au sita hivi, wapangeni hao wachangan­yeni na vijana mcheze’. Ikiwa hivyo itabidi tucheze bila kujali matokeo tutakayoyapata,” alisema kiongozi huyo’.

Tangu kutokea kwa ajali hiyo kla­bu kadhaa zimedai kuwa zipo tayari kutoa wachezaji wao kwa mkopo ku­wapa Chapecoense bure ili kumalizia ligi.

halotel-strip-1-1