×

Ummy Azindua Kitabu cha Utafiti wa Afya ya Uzazi, Mtoto

1

Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kitabu chenye matokeo ya utafiti wa afya ya uzazi na mtoto.

2

…Akisoma hotuba yake mbele ya wageni waalikwa.

3

Mkurugezi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dk. Albina Chuwa, akisoma hotuba yake.

4

Mwakilishi kutoka Umoja wa Mataifa (UN) akizungumza jambo.

5

Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia kilichokuwa kikiendelea.

6

Hafla hiyo ikiendelea.

7

Mmoja wa viongozi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu akitoa ufafanuzi wa jambo.

8

…Wageni waalikwa wakiendelea kufuatilia hafla hiyo.

WAZIRI wa wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, leo amezindua kitabu chenye matokeo ya utafiti wa afya ya uzazi na mtoto na viashiria vya malaria wa mwaka 2015/16 Tanzania.

Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam ambapo alisema takwimu hizo zinalenga kuboresha sekta ya afya katika kufikia malengo ya mama na mtoto, na ndizo takwimu rasmi za Ofisi ya Taifa ya Takwimu za mwaka 2015/16 ambapo mkazo utatiliwa katika kujadili namna ya kuboresha sekta ya afya.

Alisema takwimu hizo zinaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 42 ya wanawake wa mijini ni wanene hivyo kupaswa kuzingatia lishe na kupunguza vifo vinavyotokana na magonjwa mbalimbali yakiwemo ya kisukari na magonjwa ya moyo.

Alifafanua kwamba asilimia 21 ya wanawake wa vijijini ni wembamba na wana afya ya kawaida hivyo ipo haja kubwa ya kufanya mazoezi kwa wanawake wanene ili kuondokana na matatizo ya kiafya na matokeo hayo ni chachu katika kuboresha afya ya mama na mtoto.

Kwa upande mwingine, matokeo hayo yanaonyesha kuwa katika kaya 100 za nchini Tanzania zenye vyoo bora ni 19 wakati kaya za mijini zikionyesha asilimia 35 ndizo zenye vyoo bora kati ya kaya 100 hivyo ipo haja kubwa ya kuhakikisha wananchi wanazingatia afya ya familia ili kuondokana na magonjwa ya milipuko.

Na Denis Mtima/GPL