


Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa marehemu Mpoki Bukuku kuelekea Uwanja wa Shule ya Sekondari Tabata Kimanga, jijini Dar.

Waombolezaji wakishusha jeneza lenye mwili wa marehemu.

Waziri wa Habari, Sanaa, Vijana, Utamaduni na Michezo, Nape nnauye (kulia) akiteta jambo na Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea.

Waombolezaji wakionesha nyuso za huzuni.

Ndugu wa marehemu wakisaidiwa kufika eneo la tukio.
Waombolezaji.
Jeneza lenye mwili wa marehemu.
Katikati ni mjane wa marehemu, lilian Bukuku akiwa na watoto wake.

Mbunge wa Jimbo la Hai, Kilimanjaro, Freeman Mbowe akisalimiana na waombolezaji.
Mbowe akisalimiana na Mkurugenzi wa Radio One, Deogratius Rweyunga.

Kubenea, nape na Mbowe wakiwa kwenye maombolezo.

Mbowe akiteta jambo na Nape.
Mpoki Bukuku enzi za uhai wake.
Familia ya marehemu Bukuku wakiomboleza.

Mbowe akizungumza jambo.
Mkurugenzi Mtendaji wa The Guardian, Bwana Richard Mgamba akizungumza jambo kwa niaba ya uongozi wa Kampuni aliyokuwa akifanyia kazi marehemu Mpoki.

Steve Nyerere akizungumza jambo kwa niaba ya wasanii.
Nape akiaga mwili wa marehemu.
Mbowe akiaga.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers, Eric Shigongo akiaga mwili wa marehenmu Mpoki Bukuku.

Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete baada ya kuaga mwili wa marehemu.

Mhariri Kiongozi wa Gazeti la Championi, Saleh Ally akiaga mwili.

Waombolezaji wakiaga mwili wa marehemu.
Blogger, Issa Muhidin Michuzi akiaga.
Deo Rweyunga akipita mbele ya jeneza kuaga mwili wa marehemu.
Mtangazaji wa ITV, Sam Mahela naye akitoa heshima za mwisho.
Mtangazaji wa ITV, Abdallah Mwaipaya akiaga.
Mhariri wa Gazeti la Championi Jumatano, Phillip Nkini akiaga mwili.
Picha zote na Denis Mtima/ GPL
DAR ES SALAAM: Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye leo Desemba 26, 2016 amewaongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa mwanahabari na mpiga picha nguli, Mpoki Bukuku katika Uwanja wa Shule ya Sekondari Tabata kimanga jijini hapa.
Mbali na Waziri Nape, walihudhuria pia viongozi wengine wa Vyama, serikali na Tasnia ya Habari pamoja na Taasisi mbalimbali ambao ni, Mbunge wa Jimbo la Hai, Freeman Erikael Mbowe, Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea, Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete, Mkurugenzi Mtendaji wa The Guardian, Bwana Richard Mgamba, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers, Eric Shigongo, Mwakilishi wa Wasanii wa filamu nchini, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ na wengine.
mwili wa marehemu umesafirishwa kuelekea nyumbani kwao mkoani Dodoma kwa mazishi ambayo yanatarajiwa kufanyika kesho..
Mpoki aliaga dunia Ijumaa, Desemba 23, 2016 Katika Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (MOI), alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu baada ya kupata ajali ya kugongwa na gari maeneo la Mwenge ITV jijini Dar es Salaam.
Mpoki Bukuku amewahi kufanya kazi kama Mpiga Picha Mkuu katika gazeti la Mwananchi, Majira na Nipashe.