The House of Favourite Newspapers

Klopp: Liverpool Vs Man City ni Bonge la Mechi

 

jurgen-klopp-liverpool-thumbs-up_3412823
LIVERPOOL, 
England

KUELEKEA mechi ya Liverpool dhidi ya Manchester City, ambayo itachezwa leo Jumamosi, Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema anaamini hiyo ni mechi kubwa na hata kama yeye angekuwa shabiki asingekubali kuukosa mchezo huo.

Timu hizo zinakutana zikiwa kwenye ubora mzuri, Liverpool ikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa Premier League wakati Man City ipo nafasi ya tatu zikitofautiana kwa pointi moja tu.

Klopp alisema: “Tunataka kufikiria jinsi tutakavyojilinda kwa kuwa sisi na wao (City) wote ni wazuri wa kushambulia kwa kushtukiza.

“Sote ni wazuri wa kumiliki mpira, hivyo umakini unatakiwa kwa kuwa mwisho wa mchezo takwimu zitazungumza.

“Wao wanaimarika kama sisi tunavyoimarika tofauti na ilivyokuwa msimu uliopita, utakuwa ni mchezo mzuri, hata kama nisingekuwa natakiwa kukaa kwenye benchi ningenunua tiketi nishuhudie mchezo huu,” alisema Klopp.

Alipokuwa akiinoa Borrusia Dortmund ya Ujerumani, Klopp alikutana na Bayern Munich ikiwa chini ya Pep Guardiola ambaye ni kocha wa sasa wa Man City, mara nane, alishinda mara tatu kati ya hizo.

Comments are closed.