×

Darassa vs R.O.M.A Hatoki Mtu Mpaka Majogoo – Dar Live , Leo Usiku

roma na darassa dar live

Inatoka Gazeti la Risasi Jumamosi, Toleo la Desemba 31, 2016

HATOKI MTU! Ndiyo tafsiri nyepesi unayoweza kusema baada ya wakali wawili katika Muziki wa Hip Hop Bongo, Ibrahim Musa ‘R.O.M.A Mkatoliki’ na Shariff Thabeet ‘Darassa’ watakapovaana leo (Mkesha wa Mwaka Mpya) jukwaa moja la Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live liliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar na kufanya mpambano unaotambulika kama Nichane Nikuchane.

Darasa Asepa na Kijiji Ilala, Aonjesha Mashabiki Shoo Kali ya Bure!

Itakavyokuwa sasa

Akizungumza na Risasi Jumamosi, Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo alisema kuwa kwa upande wa maandalizi kila kitu kinaenda sawa na shoo nzima inatarajiwa kuanza mapema leo kuanzia saa saba za mchana.

“Tunaposema Mkesha wa Mwaka Mpya tunamaanisha! Sisi kama Dar Live mkesha utaanza mapema kuanzia saa saba mchana mpaka majogoo ambapo wapo wasanii kibao watakaokuwepo kama vile Topido, MC Darada pamoja na Mdogo wa R.O.M.A,” alisema Mbizo.

roma na darassa dar live

Darassa akikamua.

Wakali wengine

Mbizo aliongeza kuwa mbali na R.O.M.A na Darassa wapo wakali wengine watakaosindikiza mpambano huo.

“Tutakuwa na wakongwe wa Bongo Fleva, Sir Juma Nature na H-Mbizo, mkali wa Ngoma ya Popolipopo na Nimempata, Pam D, mkali wa Singeli, Msaga Sumu pamoja na kundi lisilo na mpinzani Bongo katika Muziki wa Taarab, Jahazi Modern.

jahaziii

Jahazi wakikinukisha.

Kiingilio je?

“Burudani zote hizo utazipata kwa kiingilio kiduchu cha shilingi 5,000 tu getini,” alimaliza Mbizo.

Msikie Darassa

Akizungumzia mpambano huo unaosubiriwa kwa hamu, Darassa anayetikisa kila kona na Ngoma ya Muziki alisema kuwa kila anapopanda jukwaani huwa hawaangushi mashabiki wake kwa kufanya miujiza ambayo haijawahi kutokea.

“Mashabiki wote wa Hip Hop na Darassa kwa ujumla hii si ya kukosa. Nitapiga nyimbo zangu zote kali kuanzia Weka Ngoma, Sikati Tamaa, Kama Utanipenda hadi hii mpya ya Muziki.

“Kikubwa niseme kwa kuchana;

‘Unataka kukimbia na hauna break,

what do you expect,

Bongo Congo kwa Thabo Mbeki,

cheza lokasi ya Mbongo uwezi kumake,

waache wa sell usije ukajicomfuse.’

roma-dar-live-5

R.O.M.A huyu hapa

Kwa upande wa R.O.M.A alisema kuwa, anaweza kufanya shoo hata kwa biti moja na akasepa na kijiji chake hivyo mashabiki wajiandae maana licha ya kuipania, amejiandaa vya kutosha na kuwaziba midomo wote wanaoona muziki wa Hip Hop haupo juu.

R.O.M.A: Darassa si Lolote si Chochote Kwangu, Atanisoma Jukwaani, Dar Live

roma na darassa dar live“Nitakuwa na sapraiz ambazo hazitabiriki, mashabiki wajiandae tu kwa ngoma kali kama Mwanakondoo, Pastor, Kaa Tayari, Una Akili Wewe pamoja na K,” alisema R.O.M.A na kuongeza

“Kitu kikubwa ambacho masha-bikiw angu wengi hawakijui, natokaga home nikiwa sijui nitafanya maajabu gani na nikifika jukwaani nachana nashangaa watu wanakuwa na mzuka wa ajabu hivyo najivunia.

roma na darassa dar liveRoma akigonga Viva Roma Viva

Kingine shoo zangu zote nikimaliza huwa narudia kuziangalia kwenye video na kufanyia marekebisho kwa hiyo niwaambie tu mashabiki wangu shoo hii itakuwa zaidi ya shoo zangu zote ulizowahi kuziona,” alimaliza R.O.M.A kwa kuachia mistari,

‘sina team nina simama wima one man army,

Wewe kimbunga mimi nakupa katrina vs sunami,

Msanii ni mvuvi mziki ndo jahazi ila kuwapata samaki ni mzikii so fanya kazi,

Sio unadis tuu na kwenye shoo unapigwa na mawe mikama umenipa nyota nina rap kisandawe (*****)

darassa-dar-live-10WAKATI HUOHUO

Jana katika Kipindi cha Uhondo kinachorushwa kupitia Redio Efm, R.O.M.A na Darassa walifunika shoo ya live ya kipindi hicho iliyofanyika katika Viwanja vya Hananasif, Kinondoni jijini Dar.

R.O.M.A aliwapagawisha kwa Wimbo wa Viva Roma Viva na Darassa Wimbo wa Muziki.

roma-na-darassa-dar-live1

Gazeti la Risasi Jumamosi, Toleo la Desemba 31, 2016

ROMA VS DARASA WALIPOKUTANA KWENYE JUKWAA LA EFM REDIO