×

Meli Yateketea kwa Moto, Watu 23 Wapoteza Maisha

meli-indonesiaShirika linalosimamia maafa nchini Indonesia limetoa taarifa kwamba takriban watu 23 wamekufa kutokana na moto uliozuka kwenye meli liiyokuwa imewabeba zaidi ya watu 200 katika Pwani ya Jakarta

Meli hiyo ilikuwa safarini kuelekea katika kisiwa cha utalii cha Tidung ambapo waokoaji bado wanaendelea kuwatafuta watu 17 ambao hawajulikani walipo.

Usafiri wa majini unategemewa sana nchini Indonesia ambapo taifa hilo lina na visiwa zaidi ya elfu 17.