×

Georgina; Huyu ndiye amemtuliza CR7

cristiano_ronaldo1Cristiano Ronaldo na mpenzi wake Georgina Rodriguez mwenye kikoti cheusi.

MADRID, Hispania| Gazeti la Championi Ijumaa, Toleo la Jan. 06, 2016

STAA wa Real Madrid, Cris­tiano Ronaldo anajulikana kwa kuwa ni mtu wa ‘totoz’, sifa hiyo alipewa kutokana na kawaida yake ya kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na wasichana wengi warembo.

Suala la kutajwa kufanya ngono au kuwa kwenye uhusiano wa muda mfupi na mrembo fulani maarufu hilo kwake siyo jambo geni.

Mrembo pekee ambaye alidumu naye kwenye uhusiano kwa muda mrefu ni Irina Shayk, mwanamitindo ambaye sasa ana umri wa miaka 30. Baada ya kutengana kwao mwaka jana, Ronaldo alikuwa kimya katika masuala ya ki­mapenzi huku ikiwa haijulikani ametulia kwa mrembo yupi baada ya hapo.

Baada ya kutulia kwa miezi kadhaa, mwishoni mwa mwaka jana, Ronaldo akaibuka na Georgina Rodriguez, mrem­bo wa Kihispania na kuwafanya watu waanze kuulizana juu ya msichana huyo.

cristiano_ronaldo2Ronaldo na Georgina walianza kuonekana pamoja wiki kadhaa nyuma wakiwa kwenye matem­bezi katika maduka kadhaa, lakini safari hii alianza kwa siri tofauti na ilivyokuwa wakati anaanza na Irina ambapo waliweka wazi mambo yao mengi.

Haya ni baadhi ya mambo ambayo yanam­husu Georgina na Ron­aldo ambaye mwezi ujao anatarajiwa kutimiza umri wa miaka 32, wakati mpenzi wake huyo ana miaka 21:

WALIKUTANA KWENYE SHOO YA MAVAZI

Walianza kukutana kwenye sherehe jijini Madrid, mrembo huyo alikuwa akifanya kazi ya masuala ya mitindo, pia alikuwa ameajiriwa katika Duka la Gucci.

Wakati anakua, Georgina ali­jifunza masuala ya kudansi la­kini baadaye akabadili na kuwa mwanamitindo.

cristiano_ronaldo3ALIMTEMBEZA MIJI TOFAUTI

Baada ya kuelewana, Ronaldo al­ianza kutoka naye na kwenye sehe­mu mbalimbali zenye mikusanyiko ya watu huku mchezaji huyo akiwa anavaa mavazi yanayoficha uso wake kwa sehemu kubwa ili kukwepa usum­bufu wa kujulikana.

Moja ya miji ambayo alimpeleka wakafurahia maisha ni Paris, Ufaran­sa ambapo walinaswa wakibusu na kuonyeshana mambo mengine ya kimahaba.

cristiano_ronaldo4MAHABA YAMEMTU­LIZA RONALDO

Inaelezwa kuwa tangu waanze kuwa pamo­ja, ki­saikolo­jia Ronaldo amet­ulia na kufanya mambo men­gikatika mstari unaoe­leweka, kiwango chake kimekuwa kizuri tofauti na mwanzoni mwa msimu al­ivyoanza.

Uwepo wa mrembo huyo uwan­jani wakati Ronaldo akicheza umeongeza nguvu kwa kuwa mara k adha a

 ame­wahi kupiga picha akiwa Bernabeu wakati Real Madrid inapocheza.

cristiano_ronaldo5Ronaldo na mpenzi wake, Georgina wakiingia kwenye hoteli ya CR7 iliyopo Funchal, Madeira

UHUSIANO WAO ULIANZA ZAMA­NI KIDOGO

Kama ilivyoelezwa juu kuwa ulian­za kwa siri, yawezekana Ronaldo maarufu kwa jina la CR7 alitaka kumsoma binti huyo kabla ya ku­fikia uamuzi wa kujionyesha naye hadharani.

Kuna picha kwenye Instagram zilizowekwa tangu Agosti mwaka jana zilithibitisha hilo, licha ya watu wengi kuanza kugundua mwisho­ni mwa mwaka jana.

cristiano_ronaldo6GEORGINA ALIZALIWA JACA

Georgina ni mzaliwa wa Jaca, huu ni mji uliopo Kaskazini Mashariki mwa Hispania, ni mwendo wa saa nne kwa gari kutoka Jiji la Madrid.

Kuna kipindi aliwahi kuishi London na kujifunza Kingereza, alipomaliza mafunzo yake hakurejea Jaca badala yake akaenda Madrid na kuanza kujihusisha na masu­ala ya mitindo.

MAISHA BINAFSI YA RONALDO

Ronaldo ni baba wa mtoto mmoja, licha ya soka anafanya biashara mbalimbali am­bazo zinasimamiwa na mama yake kwa kuwa baba yake, José Dinis Aveiro, alifariki akiwa na umri wa miaka 52 kutokana na unywaji wa pombe uliopitiliza.

Kutokana na kifo cha baba yake, Ron­aldo aliapa kutokunywa pombe. Mama wa mtoto wake hajulikani mpaka leo kwa kuwa wakati anazaliwa Juni 7, 2010 hakukuwa na taarifa za mama mtu na mpaka leo hajawahi kusema chochote. Mtoto huyo anaitwa Cristianinho.

Ronaldo ni Mkristo wa madhehebu ya Katoliki, hana tatuu mwilini kwa kuwa amekuwa akichangia damu mara kadhaa.

Penzi la Mayasa kwa Kelvin Laanza Kuota Mizizi, Global Kazini Episode 5