The House of Favourite Newspapers

Wenger: Sina Shida na Sanchez

sanchezLONDON, England

KOCHA wa Arse­nal, Arsene Wenger amesema hakuna tatizo lolote kati yake na mshambuliaji wa timu hiyo, Alexis Sanchez.

Mshambuliaji huyo wa Arsenal alionyesha kukasirika wakati al­ipotolewa uwanjani kwenye mchezo wa Ligi Kuu Eng­land dhidi ya Swan­sea, juzi Jumamosi.

Staa huyo raia wa Chile alionyesha ki­wango cha juu kwenye mchezo huo baa­da ya kufunga bao moja na kuten­geneza lingine lililofungwa na Olivier Giroud. Arsenal ilishinda 4-0.

Hata hivyo, katika dakika ya 79, Wenger alimtoa uwanjani ambapo alioneka­na kukasirika baada ya kuvua glavu zake na kuzi­piga teke kuelekea kwenye benchi la timu yake, alipofi­ka kwenye benchi akainama huku akiwa haangalii mch­ezo huo, kisha akajifunika na koti, lakini ndani ya uwanja alikuwa akiwabwatukia ho­vyo wachezaji wenzake kila walipokosea.

Tukio hili linafanana na lile ambalo alilifanya wakati wa mchezo dhidi ya Bourne­mouth wiki moja iliyopita ambao walitoka sare ya ma­bao 3-3.

“Wachezaji wote wamekuwa wakika­sirika kila wakitolewa uwanjani, wengine wame­kuwa wakionyesha wazi wengine wamekuwa wak­ificha, nipo kwenye soka kwa muda mrefu, hivyo najua.

“Nilipofanya maamuzi niliona nimefanya jambo sahihi kabisa, huyu ni mche­zaji bora ambaye amekuwa akitaka kuona timu hii in­ashinda, hakika hakuna tati­zo kati yangu naye,” alisema Wenger.

“Kila watu wana utama­duni wao. Amerika ya Kusini ni tofauti sana na Ulaya, Amerika ya Kaskazini ni to­fauti na Ulaya Kaskazini, hivyo lazima umheshimu kila mtu kulingana na uta­maduni wake.” .

Comments are closed.