×

Trump Kuwatimua Wanaoishi Marekani Kinyume cha Sheria.

jomokenyattaairportnairobi

Uwanja wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi.

Raia takriban 90 wa Somalia na  Wakenya wawili  wametimuliwa kutoka nchini Marekani saa chache baada ya taarifa kuibuka kwamba Rais Donald Trump atakabiliana na watu wanaoishi nchini humo kinyume cha sheria.

Wote wamewasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi.

jomo-kenyatta

Uwanja wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi.

Msemaji wa serikali ya Kenya Eric Kiraithe ameambia BBC kwamba raia hao wa Somalia watasafirishwa moja kwa moja hadi Mogadishu.

Trump kuwazuia wahamiaji kuingia Marekani

Rais Trump alisema Jumatano itakuwa siku muhimu kwa usalama wa Marekani.

jomo-kenyatta-1

Uwanja wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi.

Anatarajiwa kuweka masharti makali kwa raia wa mataifa saba ya Mashariki ya Kati na Afrika yenye idadi kubwa ya Waislamu wanaotafuta viza za kwenda Marekani.