Wananchi waliofika katika banda la Mahakama Kuu ya Tanzania.
WANANCHI wengi leo wamejitokeza viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupatiwa elimu ya sheria katika kuadhimisha sherehe za Wiki ya Sheria ambazo zimeanza jana na zitaendelea hadi Februari 2 mwaka huu ambapo Rais John Magufuli ataifunga rasmi katika viwanja vya Mahakama vilivyopo Mtaa wa Chimala jijini hapa.

Mkazi wa jiji la Dar (kulia) akipatiwa elimu ya sheria kutoka kwa, Ofisa Mradi, Asha Komba wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA).
Kamera yetu ilipita maeneo hayo na kuwashuhudia baadhi ya wananchi wakipata huduma mbalimbali ya elimu juu ya sheria.

Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kitengo cha Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Charles Magesa, akiwafafanulia jambo baadhi ya waandishi wa habari waliofika kwenye banda hilo.
Wiki iliyopita wakati Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma akizungumza na wanahabari alisema kuwa miongoni mwa huduma zitakazotolewa katika wiki ya sheria ni pamoja na taratibu za ufunguaji mashauri katika ngazi mbalimbali za mahakama, taratibu za kesi za dhamana, taratibu za rufaa, taratibu za kesi za mirathi ndoa na talaka, taratibu za kupokea na kushughulikia malalamiko na msaada wa kisheria.

Mmoja wa wakazi wa jiji la Dar aliyefika katika banda hilo akimuuliza jambo Ofisa Uchunguzi Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Aristarico Majura (aliyeko mbele).
Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini mwaka huu yanakuja na kaulimbiu isemayo ‘Umuhimu wa Utoaji Haki kwa Wakati Kuwezesha Ukuaji wa Uchumi’.

Wananchi wakiendelea kupatiwa elimu juu ya haki za kisheria.
NA DENIS MTIMA/GPL