×

Kopa, Mwanahawa Kukutana Valentine Dar Live

Khadija Kopa katikati akitumbuiza.

Showbiz-XTRA |AMANI

WAKONGWE wawili kunako muziki wa Taarab, Mwanahawa Ally kutoka East Africa Modern pamoja na Khadija Kopa kutoka TOT wanatarajiwa kukutana uso kwa uso Sikukuu ya Wapendanao ‘Valentine’s Day’ itakayofanyika Februari 14, mwaka huu ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar. 

Mwanahawa akitumbuiza

Akizun-gumza na Showbiz- Xtra, Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo alisema kuwa usiku huo wapendanao 100 watakao-pendeza watapata zawadi spesho huku wakipata huduma bora ya V.I.P.

“Tutakuwa na zawadi nyingi za kuwapa wapendanao kwa sababu siku yenyewe ni spesho. Niwaombe wajitokeze kwa wingi kwani Dar Live tumewaandaliwa vitu vingi vinavyoambatana na wakongwe wawili ambao hawashikiki katika Muziki wa Taarab,” alisema Mbizo.

Khadija Kopa anatamba na vibao vingi vikiwemo Mjini Chuo Kikuu na Fahari ya Mwanamke wakati Mwanahawa Ally akitamba na vibao kama Wakerekwao, Wema na Roho Mbaya Haijengi