Mr. Shinda Nyumba Aibukia Ilala, Kigogo na Mbagala
Global Publishers February 6, 2017
SHARE THIS:
Wafanyabiashara wa Soko la Kigogo Sambusa jijini Dar wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mr. Shinda Nyumba baada ya kujaza kuponi za Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili.Afisa Masoko wa Global Publishers, Jimmy Haroub (kulia) akimuelekeza mkazi wa Ilala Mchikichini Dar, jinsi ya kushiriki Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili.Wakazi wa Mtoni Kijichi wakiweka kuponi kwenye ndoo tayari kwa ajili ya bahati nasibu hiyo inayotarajiwa kuanza kuchezeshwa droo ya kwanza leo katika Viwanja vya Mbagala Zakhem jijini Dar.Wafanyabiashara wa Keko Fenicha wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mr. Shinda Nyumba baada ya kujaza kuponi.
Jimmy Haroub (kulia) akimkatia kuponi mmoja wa wasomaji wa magazeti ya Global baada ya kumaliza kuijaza.Mr. Shinda Nyumba akimuelekeza mmoja wa wasomaji jinsi ya kushiriki bahati nasibu hiyo.
Mr. Shinda Nyumba amewatembelea wasomaji wa Magazeti yanayochapishwa na Kampuni ya Global Publishers (Amani, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Risasi, Risasi Mchanganyiko, Championi na Uwazi) maeneo ya Ilala, Mbagala na kigogo jijini Dar na kufanikiwa kuzungumza nao huku akiwasisitiza kununua magazeti hayo na kuzaja kuponi ili washiriki Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili.
Kushiriki Shinda Nyumba, nunua gazeti lolote la global Publishers kwa Tsh. 500 tu, jaza kuponi iliyoko ukurasa wa pili wa magazeti yaliyotajwa hapo juu na ufuate maelekezo. Mshindi ataibuka na nyumba mpya yenye kila kitu ndani.
Droo ya kwanza ya Shinda Nyumba itafanyika Jumatano Februari 8, 2017 ambapo zawadi kibao zitatolewa.
Nunua magazeti ya Globa Publishers ujaze kuponi na ushinde nyumba.