
MKUU wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema leo amezindua kampeni maalum ya kufanya mazoezi katika wilaya yake ambapo wananchi watakuwa wakifanya mazoezi hayo kila mwisho wa mwezi.






Akiizungumza kampeni hiyo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar, mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba mazoezi hujenga afya bora lakini pia huzuia magonjwa nyemelezi hivyo ni muhimu sana kila mwananchi kuhakikisha anafanya mazoezi kwa ajili ya afya.
Kauli mbiu ya kampeni hiyo inasema Afya ni Mtaji wa Maendeleo, Nitailinda kwa Gharama Nafuu kwa Kufanya Mazoezi
NA DENIS MTIMA/GPL
Kwa stori zote kali, Tu-follow
Facebook @Globalpublishers
Twitter @GlobalHabari
Instagram @GlobalPublishers
YouTube @GlobalTVTZ