
Taharuki imeibuka leo mchaana baada ya Jengo la Water Front lililopo pembezoni mwa Bandari Kuu ya Dar es Salaam kudaiwa kuwaka moto huku watu waliokuwemo ndani wakikimbia kuokoa uhai wao.

Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, lililazimika kuifunga kwa muda Barabara ya Sokoine kufuatia ajali hiyo.

Walinzi wakikagua wanaotoka nje ya jengo hilo.




Waziri wa Biashara, Viwanda na Uwekezaji, Eng. Charles Mwijage ambaye pia ofisi yake ipo ndani ya jengo hilo akiwa nje akitaharuki.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, chanzo cha moto huo kimeelezwa kuwa ni pikipiki ya magurudumu matatu (bajaji) ya serikali ambayo ilikuwa imeegeshwa kwenye eneo maalum la maegesho ndani ya jengo hilo na muda mfupi baadaye ikasababisha moto ulioanzia katika betri.

Ikumbukwe kuwa ni mara ya pili jengo hilo kupatwa na ajali hii.





Taharuki ikitanda miongoni mwa watu waliokuwa eneo la tukio.
PICHA: NA DENIS MTIMA | GLOBAL PUBLISHERS