×

Mtanzania Ashika Nafasi ya Pili Tuzo za DStv Eutelsat Star

Mshindi wa Dstv Eutelsat Stars Awards, Devids Bwana akizungumza jambo

DAVIDS Bwana mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Feza amefanikiwa kuibuka mshindi wa pili barani Afrika wa kuandika insha juu ya mambo ya utaalamu wa anga, tuzo ambazo zinazoandaliwa na Multi Choice Afrika kwa kushirikiana na Shirika la Anga la Eutelsat.

…Devids (wa tatu kukoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wenzake mzazi wake na maafisa Mbalimbali kutoka Dstv.

Shindano hilo lilifanyika Februari 7, Lagos, Nigeria ambapo washindi walitangazwa baada ya kamati inayohusika na mashindano hayo kukutana mjini humo chini ya mwanamama Claudie Haignere.

Mama mzazi wa Davids aitwaye Dk Esther Mbutolwe akizungumza jambo.
Meneja Masoko wa Dstv,  Alphar Mria akimpa mkono wa pongezi Devids
..akimuelezea mwanaye jambo

 

Tuzo za Dstv Eutelsat Star Awards 2017 niza mara ya sita kufanyika zikishirikisha takribani shule 1,000 kutoka nchi  20 barani Afrika na miongoni mwa nchi hizo ni pamoja na Tanzania , Nigeria Ethiopia na Botswana.