
Na ANDREW CARLOS| IJUMAA WIKIENDA| OVER ZE WEEKEND
ZIKIWA zimepita wiki kadhaa tangu msanii wa Bongo Fleva, Barnabas Elius kudaiwa kutengana na mzazi mwenziye, msanii wa Bongo Fleva, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ amemfungukia kuwa, ishu hiyo alipoisikia ilimshtua sana.

Akichonga machache na Over Ze Weekend, Lulu Diva anayetamba kwa sasa na Ngoma ya Usimwache iliyofanyika MJ Records chini ya Daxo Chali alisema, amekuwa na Barnaba kwa ukaribu kwa muda mrefu na taarifa za kuachana na mzazi mwenziye huyo zilimshtua.

“Kama utakumbuka hata wimbo wangu wa kwanza kuutoa (Milele) niliandikiwa na kushirikiana kwa asilimia kubwa na Barnaba so utaona ni jinsi gani alivyokuwa muhimu kwangu.
“Ishu hii nilivyoisikia nilimpigia na kumuuliza; braza vipi tena mbona mitandaoni unachafuka sana, akasema waache tu waongee wataacha wenyewe,” alisema Lulu. Hivi karibuni, taarifa na picha zilizagaa mitandaoni kuwa, Barnaba ameachana na mzazi mwenziye chanzo kikiwa ni kufumania picha