×

Jukwaa la Wahariri Laamuru Vyombo Vyote vya Habari Nchini Kutofanya Kazi na RC Makonda


 

Jukwaa la Wahariri Tanzania, leo Machi 22, 2017 limelaani kitendo kilichofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuvamia Kituo cha Televisheni cha Clouds TV na kudaiwa kushinikiza kurushwa hewani kwa kipindi chake.

Aidha Jukwaa hilo limetangaza vyombo vyote vya habari Tanzania wasishirikiane na mkuu huyo wa Mkoa, kutoandika habari zinazomhusu wala kurusha matangazo yake ambapo uamuzi huo utaanza kutekelezwa mara moja.

“Katika hili waandishi,wahariri wote tunakubaliana, sote tunasema halikubaliki na tunalaani vikali vitendo vya Makonda.

“Tunaalani vitendo vya Makonda na atakayekiuka na kufanya kazi na Makonda, kitakachomkuta hatutamsaidia, waandishi, wahariri wote tunakubaliana, sote tunasema halikubaliki na tunalaani vikali vitendo vya Makonda.

“Utekelezaji agizo la kutokufanya kazi na RC Dar unaanza mara moja kwa vyombo vyote vya habari nchini – Jukwaa la Wahariri.

SIKILIZA ALICHOKISEMA NAPE BAADA YA KUKABIDHIWA RIPOTI SAKATA LA MAKONDA VS CLOUDS