The House of Favourite Newspapers

BMT Wja na Tamasha la Wanawake

Na Ibrahim Mussa/CHAMPION/GPL

BARAZA la Michezo la Taifa (BMT), linatarajia kufanya tamasha la michezo kwa wanawake na wasichana lililopangwa kufanyika Aprili 8, mwaka huu kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar.

Tamasha hilo litaanza na kongamano la akina mama wanamichezo ambalo litalenga nafasi ya mwanamke katika maendeleo ya michezo na uongozi nchini.

Mjumbe wa kamati ya utendaji wa baraza hilo, Jennifer Shang’a, amesema:

“Lengo kubwa la kufanya tamasha hili ni kuweza kuhamasisha ushiriki wa wasichana na wanawake katika michezo na uongozi ili kuweza kuleta maendeleo ya haraka.

Katika tamasha hili, washiriki ni wasichana wa shule za msingi, sekondari, vyuo mbalimbali, wanawake kutoka wizara za serikali, asasi za kiraia, viongozi wa serikali, taasisi za ndani na za kimataifa ambapo kutakuwa na matembezi na michezo mbalimbali.”

Comments are closed.