The House of Favourite Newspapers

Patcho Mwamba Kujikita Kotekote

0

Stori: Issa Mnally | RISASI MCHANGANYIKO| RISASI VIBES

MWANAMUZIKI nguli wa Bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma,’ Patcho Mwamba amesema mwaka huu atahakikisha anajikita vizuri kwenye fani za muziki na filamu ili aweze kukabiliana na maisha ya sasa.

Akizungumza na Risasi Vibes katika Ukumbi wa Msasani Club, jijini Dar, Patcho alisema ameamua kufanya hivyo baada ya kugundua ana mashabiki wengi pia katika filamu.

“Unajua wakati ule nilikuwa naigiza kama sehemu ya kuzugia tu, sasa nimeamua kuingia mzimamzima katika filamu huku nikiendelea na muziki, maana nimeona nina mashabiki pia kwenye filamu,” alisema Patcho.

Leave A Reply