×

Msuva Ataja Dakika 450 za Kifo

Mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva.

Said Ally | Championi Ijumaa | Habari

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva, ameweka wazi kuwa watapambana kwa ajili ya kuhakikisha timu yao inaipiku Simba katika vita ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu, akasisitiza lazima wafanye kweli katika michezo yao mitano waliyobakiza ambayo ni sawa na dakika 450.

Kwa sasa Yanga wanautolea macho ubingwa wa ligi kutokana na kuwa kombe pekee lililobaki ambalo wanaweza
kulitwaa baada ya hivi karibuni kuondoshwa kwenye Kombe la FA na Mbao ya Mwanza.

Kiungo huyo mwenye mabao 12 kwenye ligi ameliambia Championi Ijumaa kuwa wanaelekeza nguvu zaidi katika ligi kwa nia ya kuchukua ubingwa ili kuwapoza machungu mashabiki wao pamoja na kurudisha mataji ndani ya timu hiyo.

“Hizi mechi tano ndizo za kuzifanyia kazi kuhakikisha kwamba tunachukuaubingwa iwe isiwe, kwa sababu ndilo kombe ambalo tunalitolea macho baada ya kutupwa nje ya makombe yote mengine tunayoshiriki.

“Naamini kila mmoja atajitoa kwa uwezo kulifanikisha dhumuni hilo kwa ajili ya kuwapa furaha mashabiki wetu lakini pia kurejesha makombe ambayo kama hatutayakazania basi tunaweza kuyapoteza yote ndani ya msimu huu,” alisema Msuva.

Spoti Hausi LIVE: Binslum Afunguka Udhamini Wake Kwenye Soka la Bongo

Leave a Comment