×

Kiongozi wa Washia Aomboleza Vifo vya Wanafunzi Arusha

Kiongozi mkuu wa Waislam wa madhehebu la Washia nchini, Sheikh Hemed Jalala.

Kiongozi mkuu wa Waislam wa madhehebu la Washia nchini, Sheikh Hemed Jalala, ametoa pole kwa wafiwa wote wa ajali iliyotokea Karatu mkoani Arusha na kusababisha vifo vya wanafunzi  32 na walimu wa shule ya St. Lucky Vincent.

Shekh Jalala amesema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa  Waislam wa madhehebu ya Shia wamesikitishwa na kushtushwa na msiba huo na wanaungana na Waislam  wenzao, Wakristo   na Watanzania wote kwa msiba huo mkubwa.

Aidha ametoa pole kwa  wazazi na walezi wa watoto hao na kwa Rais Dk. John Magufuli kwa msiba huo mkubwa katika taifa letu.

Na Denis Mtima|GPL

Leave a Comment