The House of Favourite Newspapers

Wema Sepetu Aibua Ishu Kwa Mume wa Mtu!

0
Staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu.

STORI: HAMIDA HASSAN NA GLADNESS MALLYA| RISASI JUMAMOSI | HABARI

DAR ES SALAAM: Kuna ishu! Ndivyo wasemavyo wapenda ubuyu kufuatia ukaribu wa staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu na mume wa mtu anayejulikana kwa jina la Daudi Mambya baada ya kunaswa wakiwa pamoja kwenye matukio kibao, Risasi Jumamosi linakupa habari kamili. Kwa mujibu wa watu hao, wawili hao wamekuwa wakionekana wakiwa ‘veri klozi’ kila anapokwenda Wema hasa mahakamani kwa ajili ya kesi inayomkabili ya kutumia na kukutwa na madawa ya kulevya.

Imeelezwa kuwa, mara zote ambazo Wema alitinga katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu jijini Dar kwenye kesi hiyo, aliambatana na Daudi hivyo watu kuanza kuhoji ‘sivii’ ya jamaa huyo kwa Wema ilihali kila mtu anajua ni mume wa mtu. Chanzo makini kililieleza Risasi Jumamosi kuwa, huenda wawili hao wana kitu nyuma ya pazia kwa sababu Daudi amekuwa mstari wa mbele kuhudhuria mahakamani tofauti hata marafiki wa karibu na Wema.

“Yaani huyu Daudi ambaye ni mume wa mtu, kila Wema akienda mahakamani lazima naye awepo pembeni yake kumsindikiza, jambo hili limezua maswali kwa watu kibao na kusema huenda anammiliki mwanadada huyo maana siyo kawaida kwa mtu mwenye kazi zake kupoteza muda kwenda kumsindikiza tu mtu ambaye hamhusu,” kilidai chanzo hicho.

Baada ya Risasi Jumamosi kunasa matukio tofauti ya Wema na Daudi wakiwa pamoja kwa siku tano tofauti, paparazi wetu alimtafuta Daudi ambaye alikiri kwenda mahakamani kila kesi ya Wema inapotajwa kwa kuwa ni rafiki yake na hawezi kumuacha akiwa na matatizo.

“Sina undugu na Wema ila ni rafiki yangu sana na sina uhusiano naye wa kimapenzi kama watu wanavyodai, unajua urafiki mzuri ni ule mnaosaidiana katika shida na raha hivyo siwezi kumtenga au kumuacha Wema wakati huu wa matatizo ilihali wakati wa raha tulikuwa marafiki.

“Wema kipindi hiki amejua kuwa hana marafiki wa kweli maana rafiki wa kweli ni yule mnayesaidiana katika shida na raha ndiyo maana mimi nikaamua kuwa naye kwani najua maana ya urafiki, anao wengi, lakini wapo wanaomjua wakati wa raha tu,” alisema Daudi huku Wema akigoma kupokea simu kila ilipopigwa.

Leave A Reply