×

Droo Ndogo ya Nne ya Shinda Nyumba Sasa Mei 31

Mr. Shinda Nyumba akiwaelekeza wasomaji namna ya kujaza kuponi za Shindano la Shinda Nyumba

DROO ndogo ya nne ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awa­mu ya Pili imewadia na sasa itafanyika Mei 31, mwaka huu na kama kawaida washindi watapata zawadi mbalimbali ikiwemo ile kubwa ya pikipiki.

Muuzaji wa magaezti ya Kampuni ya Global Publishers akiwaelekeza wasomaji namna ya kushiriki Shinda Nyumba

Afisa Masoko wa Kampuni ya Global Publishers, inayoende­sha bahati nasibu hiyo, Yohana Mkanda alisema kuwa baada ya kufanya droo tatu ndogo kwa mafanikio makubwa, sasa inakuja ya nne ambayo itafanyika mwis­honi mwa mwezi huu katika eneo ambalo bado linafanyiwa kazi.

“Tuna uhakika wa kufanya droo hiyo mwisho wa mwezi huu, lakini kuhusu wapi tutalifanyia zoezi hilo, bado tunaendelea na mazungumzo na mara itaka­pokamilika, tutawafahamisha wasomaji wetu ili wajiandae kwa shughuli hiyo.

 

Washindi wa zawadi mbalimbali wa droo ya tatu ya Shinda Nyumba.

“Kama wanavyojua tumeanza kuboresha zawadi zetu kwa kadiri tunavyokwenda, katika droo zetu tatu ndogo ambazo tumeshazi­fanya, jumla ya pikipiki tatu zime­shatolewa, televisheni kubwa flat screen tatu pia, dinner set tatu na simu za kisasa nyingi tu.

“Tunawasihi waendelee kusoma magazeti yetu ambayo licha ya bahati nasibu hiyo, pia yanawaletea habari motomoto za kijamii, michezo, burudani na mastaa mbalimbali.

“Katika magazeti yetu yote, kwenye kurasa za pili zipo kuponi zenye maelekezo ya namna ya kufanya, wakishamaliza kujaza, wanaweza kuzituma kwetu kupi­tia kwa mawakala wetu waliopo nchi nzima na wale wa Dar es Salaam wanaweza kuja ofisini kwetu, Bamaga Mwenge na kuzi­acha kwenye ndoo ya kukusanyia kuponi,” alisema Mkanda.

Bahati Nasibu ya Shinda Ny­umba Awamu ya Pili imedhamin­iwa na Kampuni ya Tecno Mobile, King’amuzi cha Ting, British School na Kilimanjaro Institute of Technology.

Leave a Comment