×

SportPesa, Everton Wajionea Vipaji vya Soka kwa Vijana Nchini

Leon Osman akisalimiana na vijana wanasoka wa Tanzania katika Uwanja wa Taifa
Nahodha wa zamani wa Klabu ya Everton ya Uingereza, Leon Osman yuko nchini katika ziara fupi iliyoratibiwa na Kampuni ya Michezo ya Kubahatisha ya SportPesa.
Leon Osman akisalimiana na vijana, kulia ni Waziri wa Habari, Vijana, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe.
Leon ameongozana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Everton, Robert Elstone ambaye kitaaluma ni mhasibu.

Kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Osman amepata nafasi ya kuona baadhi ya wachezaji wenye vipaji ambao walialikwa na kucheza na mpira.

Kati ya watu waliokuwepo uwanjani ni mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe. Pia Ofisa Mtendaji Mkuu wa SportPesa Tanzania, Pavel Slavkov.

Osman aliichezea Everton katika Ligi Kuu England na michuano mingine tokea mwaka 2000 hadi 2016 alipotangaza kustaafu akiwa mmoja wa manahodha.
Dkt. Harrison Mwakyembe akibadilishana mawazo na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Everton, Robert Elstone.

PICHA NA MUSA MATEJA | GPL

Leave a Comment