KWA sasa hakuna ubishi mchezaji bora zaidi katika mpira wa kikapu kuwa ni LeBron James wa Cleveland Cavaliers. Katika fainali za NBA za mwaka huu, LeBron anafanya kazi ya ziada kuiongoza Cavaliers dhidi ya kikosi cha Golden State Warriors wenye nafasi kubwa ya kuwa mabingwa mwaka huu.

Mpaka sasa Golden State Warriors wanaongoza kwa kushinda mechi tatu dhidi ya nne walizocheza huku Cleveland Cavaliers wakishinda moja usiku wa kuamkia leo.