×

Beyonce, Jay-Z Wafurahia Watoto Mapacha Huko Los Angeles

Jay-Z akiwa na mkewe, Beyonce, wakati akingali mjamzito.

MWANAMUZIKI mshindi wa tuzo ya Grammy, Beyonce, na mumewe rapa, Jay-Z,  Jumatatu au usiku wa kuamkia Jumanne wiki inayomalizikia leo, waliwakaribisha watoto wao mapacha waliozaliwa katika hospitali moja jijini Los Angeles.

Habari zilizopo ni kwamba wanamuziki hao wanaojulikana kwa kifupi kama Bey na Jay,  wamefurahishwa vikubwa na habari hizo ambazo wanawajulisha ndugu na marafiki sehemu mbalimbali.

Wawili hao waliooana mwaka 2008 na ambao tayari wana mtoto wa kike aitwaye Blue Ivy mwenye umri wa miaka mitano, wanasemekana kupata mapacha wa kiume na kike.

1 Comment

Leave a Comment