
Wasomaji wa magazeti ya Global Publishers ambayo ni Amani, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Risasi, Uwazi, na Championi wa pande za Tegeta na viunga vyake jana Alhamisi, waliibukiwa na Mr. Shinda Nyumba aliyekuwa na timu nzima ya promesheni ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba.

Mr. Shinda Nyumba akiwa na timu yake walianzia Njia ya Panda ya Kunduchi (Mbuyuni) kunadi gazeti la Amani sambamba na magazeti mengine ya Global yenye kuponi ambayo msomaji alitakiwa kununua gazeti, kuijaza na kuikata kuponi kisha kuipa timu ya msafara huo.

Wasomaji hao walionesha furaha yao kwa msafara huo na kuanza kuchangamkia gazeti la Amani ambalo linakuwa mtaani kila Alhamisi na kujaza kuponi kila mmoja akijaribu bahati yake kuweza kujishindia nyumba mpya na samani zake ndani hiyo na zawadi zingine ikiwemo simu za kisasa ‘smart phone’, ving’amuzi vya Ting, Dinner Set na pikipiki.

Baada ya kuagana na wasomaji hao msafara huo ulielekea maeneo ya Tegeta hadi Bunju na viunga vyake, kisha ukaenda kumalizia mzunguuko wake eneo la kiwanda cha saruji cha Wazo Hill ambapo umati wa wasomaji waliokutwa eneo hilo walianza kuchangamkia magazeti hayo.

Baadhi ya wasomaji hao walionekana kuvutiwa na muonekano wa Mr Shinda Nyumba na kuamua kupiga nae picha za Selfie kwa ajili ya kumbukumbu zao.




Na Richard Bukos