×

Mcongo; Historia ya ‘Rumble In The Jungle’ itanibeba Dar Live

Mikanda ya Ubingwa wa Global TV Online.

 

KATIKA historia ya mchezo wa ngumi za kulipwa duniani, DR Congo inakumbukwa kutokana na kufanyika kwa pambano kubwa la uzito wa juu kati ya Muhammad Ali ‘The Greatest’ dhidi ya George Foreman wote wakiwa ni Wamarekani.

 

Katika pambano hilo lililofanyika Oktoba 30, mwaka 1974 kwenye Uwanja wa Stade du 20 Mai, Kinshasa, ambalo lilipewa jina la ‘Rumble in the Jungle’ Ali alishinda dhidi ya Foreman kwa KO katika raundi ya nane, pambano likiwa ni la raundi 15 ambapo moto wake haukuwa wa kitoto.

Idd Pialali: Njooni Dar Live Mshuhudie Nitakavyomuua Mkongo

 

Mwadziwana.

 

Huenda hii ikajirudia Julai 22, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Dar Live pale bondia kutoka DR Congo, Regin Champion atakavyoonyeshana umwamba na Mtanzania Idd Pialali katika pambano la kimataifa la kugombania Ubingwa wa Global TV, Afrika Mashariki na Kati ambalo litarushwa mubashara na kituo cha Global Tv Online kupitia website yake ya www.globaltvtz.com.

 

Mapambano mengine yatakuwa ni kati ya bondia, Francis Miyeyusho ‘Chichi Mawe’ atakayezichapa na Israel Kamwamba raia wa Malawi, wakati Nasibu Ramadhan ‘Pacman’ akitarajia kucheza na Tinashe Mwadziwana kutoka nchini Zimbabwe. Mapambano hayo yote ni ubingwa wa Global TV, Afrika Mashariki na Kati na yatakuwa ni ya raundi kumi.

 

Ibrahimu Class ‘King Class Mawe’.

 

Risasi Mchanganyiko limefanya mahojiano maalum na bondia kutoka DR Congo, Regin Champion kuelekea pambano hilo ambaye amejivunia historia iliyoachwa na mabondia waliokuwa na rekodi za kutisha katika mchezo huo ambao waliopigana katika ardhi ya nchi yake.

 

Champion alianza kwa kusema: “Baba yangu ndiyo sababu kubwa iliyopelekea nicheze ngumi za kulipwa hapa kwetu DR Congo, yeye ndiyo aliniambia nicheze mchezo huu, nashukuru mpaka leo bado nacheza bila ya tatizo lakini pia naupenda kwa sababu umenipa mafanikio.

 

Championi.

 

“Nimecheza mapambano mengi, nimeshinda mengi na nimepoteza mechi tatu katika mapambano niliyocheza, sitaki kusema sana lakini huyo mpinzani wangu (Pialali) nitampa raundi tatu pekee za kucheza na kitakachofuatia kutoka hapo ni kichapo kikali.

 

“Nadhani shida yangu kubwa ni kushinda huo Ubingwa wa Global TV, Afrika Mashariki na Kati kwa sababu nimeshacheza Zambia, Angola, Zimbabwe, Msumbiji , Malawi na hapa kwetu Congo nimeshacheza nyingi, mimi ni bingwa wa hapa DR Congo.

Kamwamba.

 

Unakuja kucheza ugenini, labda una kipi cha kuwaambia?

“Kiukweli nitashukuru kwanza kwa Watanzania ambao watanisapoti pamoja na Wacongo wote ambao wanaishi huko naomba wanipe ushirikiano ndugu yao, nakuja Tanzania kwa ajili ya kumchakaza mpinzani wangu.

 

“Mpinzani wangu simjui kabisa na naamini pia hanijui, lakini kutokana na maandalizi ambayo naendelea kuyafanya huku kwetu, sina hakika kama ataweza kutoka kwa sababu siku zote huwa sipendi mchezo ninapokuwa juu ya ulingo, kwani kazi yangu ni kuchapa tu.

 

“Sihofii chochote kuhusu yeye, kikubwa nadhani ajipange kwa sababu huenda akawa anafikiria kuwa Champion ni bondia wa kawaida ila nataka nimwambie ajue kuwa tutajuana vizuri kwenye ringi, kiufundi na kimbinu maana siwezi kukubali kupigwa kirahisi hasa ukilinganisha na umbali wa sehemu niliyotoka.

 

Pacman.

 

“Najua ngumi ni vita ambayo inakuwa ya watu wawili wakipigana kwa mikono sasa nipo tayari kuona nasitisha uwezo na kipaji cha mpinzani wangu katika raundi chache za mwanzoni kwa kumpoteza kabisa, hilo anapaswa kulijua hata kama atakuwa anacheza katika ardhi ya kwao.

 

“Lakini nimeambiwa kuwa katika ukumbi hakutakuwa na mashabiki wengi kwa sababu litarushwa live na kituo cha Global TV Online, ni kitu kizuri hasa kwa upande wangu kwa sababu mashabiki wangu na Wacongo wataweza kuona nitakachokuwa nakifanya katika ulingo huko.

Idd Pialali.

“Nimeomba nipewe ‘links’ mapema kwa ajili yao ili waanze mara moja kujiweka tayari kushuhudia mambo ya kutisha nitakayoweza kuyafanya, naamini historia ya pambano la Muhammad Ali na George Foreman ambao walicheza kwenye ardhi yetu itanibeba licha ya kusimuliwa na kuisoma tu.

 

Katika hatua nyingine, pambano hilo, hakutakuwa na kiingilio na mashabiki wataweza kulishuhudia mubashara kupitia simu zao za mkononi, kwani litaonyeshwa na Global TV pekee. Wadau na mashabiki watakaopata nafasi ya kuingia ukumbini wataingia kwa kadi maalum za mwaliko tu.

 

Ili kulishuhudia pambano hilo kwa njia ya simu tena bure, hakikisha unajiunga (SUBSCRIBE) na YouTube Chanel ya Global TV Online sasa hivi ili usipitwe. Ingia You Tube, tafuta GLOBAL TV ONLINE, kisha bonyeza neno subscribe pia bonyeza kikengele kidogo kilichopo pembeni yake ambacho kitakukumbusha kuangalia pambano hilo mara tu litakapoanza.

 

Kama wewe umeshajiunga, basi hakikisha pia umebonyeza kikengele ili usipitwe na kila kinachoendelea Global TV. Pia unaweza kutupata kupitia mtandao wa www.globaltvtz. com, jiunge sasa na Global TV ili uwe wa kwanza kuona ndondi za kimataifa. Jiunge sasa kwa kuingia www. youtube.com/user/uwazi1.

 

Makala: Ibrahim Mussa | RISASI MCHANGANYIKO

Video: Nasib Ramadhani Nitampiga vibaya Mzimbabwe Njooni Dar Live

Leave a Comment