×

Barthez: Nimekuja Kuipa Mafanikio Singida

Aliyekuwa kipa wa Yanga, Ally Mus­tafa ‘Barthez’.

KATIKATI ya wiki iliyopita, Klabu ya Singida United ilikamilisha dili la kumsajili kipa wa Yanga, Ally Mus­tafa ‘Barthez’ kwa kumpa mkataba wa miaka miwili.

Barthez ame­jiunga na Singida baada ya kumaliza mkataba wake ndani ya Klabu ya Yanga huku akionekana hana tena nafasi ya kuendelea kuichezea timu hiyo chini ya benchi la ufundi linaloongozwa na Mzam­bia, George Lwandamina.

Msimu ujao kipa huyo atakuwa akifundishwa na kocha wake wa zamani aliyekuwa naye Yanga, Mholanzi, Hans van Der Pluijm.

Kipa huyo ambaye pia aliwahi kuichezea Simba, amefanya ma­hojiano maalum na Championi Jumatatu na kuzungumza mambo mengi na sababu hasa iliyomfanya ahamie Singida United inayod­haminiwa na Kampuni ya Michezo ya Kubashiri ya SportPesa.

K W A N I N I U M E O N ­DOKA YAN­GA?

“Muda wa kuondoka ulifika ndiyo maana nikafanya hivyo.

“Najua Yanga ni timu kubwa na ilinipa kila kitu nilichokuwa nikihitaji, ukian­galia mataji ya Ligi Kuu Bara, Kombe la FA hata Ngao ya Jamii nimechukua nikiwa Yan­ga bila kusahau kushiriki mi­chuano ya kimataifa, hivyo sikuwa na sababu ya kuendelea kung’ang’ania s e ­hemu moja wakati nimeshapata kila kitu.

Barthez akiongea na moja wa viongozi wa benchi la ufundi la Singida United.

NI NINI HASA KIMEKU­FANYA UJIUNGE NA SINGIDA NA SIYO TIMU NYINGINE?

“Ni kutokana na maa­muzi yangu si kitu kingine, una­jua kila mtu huwa na maamuzi yake, kwa hiyo binafsi niliona huu ni muda sahihi wa mimi kuja huku kwa sababu wao wenyewe walionyesha nia ya kunihitaji zaidi.

“Lakini pia ukiangalia hii timu imejipanga kweli ku­leta changamoto mpya ka­tika ligi yetu, nikiwa kama mchezaji huwa napenda kucheza timu yenye ku­leta ushindani.

“Na jambo kubwa am­balo ninalotaka kulifanya hapa ni kuipa timu ma­fanikio kama yale niliy­oyapata nikiwa Yanga.

U N A J I S I K I A J E KUFUNDISHWA TENA NA PLUIJM?

“Ni vizuri tu kwa saba­bu tangu nianze kufan­ya naye kazi nimeona ni kocha mzuri am­baye anapenda timu yake ifanikiwe muda wote. Kutokana na hilo naamini huku pia tuta­fanikiwa chini yake.

WEWE NA NIZAR KHALFAN NDI­YO WAKONGWE HAPA, UNAWAAM­BIA NINI VIJANA WALIOSALIA?

“Tushirikiane tu kuijenga timu na naamini ukongwe wetu tutautumia vizuri kuwapa hamasa hawa wenzetu ili tu timu ifanye vizuri.

UNA LIPI LA KUWAAMBIA MASHABIKI WA SINGIDA UNITED

“Wanachotakiwa ni kuendelea kuisapoti timu yao wakati wote ili tuweze kufikia malengo ambayo yapo kwani hapa kila mmoja ana­hitaji nguvu ya mwenzake kufan­ikisha jambo.

NENO LOLOTE KWA SOKA LA BONGO

“Nadhani kila siku kuna mabadi­liko, nauona msimu ujao ukiwa na ushindani mkubwa kutoka­na na timu kujipanga vizuri.

“Ukiangalia zamani Simba, Yanga na Azam ndizo zili­zokuwa zinaonekana kuwa vizuri pekee, lakini naamini msimu ujao Singida nayo itakuwa katika kundi hilo.

“Nasema hivyo kutokana na kwamba huu udhamini ulioletwa na SportsPesa umechangia timu ku­jengeka vizuri,” anase­ma Barthez.

Kumbe Top 5 Ya Wasanii wa BSS 2015, Waliachwa Kwenye Mataa,Ukweli Huu Hapa

Leave a Comment