×

Video: Ofisi za IMMMA Advocates Zateketea Kwa Moto


Ofisi za IMMMA Advocates zinazomilikiwa na  wanasheria Fatuma Karume na Lawrence Masha zilizopo Upanga jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo zimeteketea kwa moto baada ya kutokea kwa mlipuko wa kitu ambacho mpaka sasa hakijafahamika.

https://globalpublishers.co.tz/polisi-yaanza-kuchunguza-mlipuko-ulioteketeza-ofisi-za-mawakili

Taarifa kutoka eneo la tukio, zinaeleza kwamba kabla ya tukio hilo, walinzi wawili waliokuwa wakilinda ofisi hizo, kutoka Kampuni ya Knight Support, walinyweshwa kitu kinachodaiwa kuwa ni sumu na baadaye wakaenda kutupwa eneo la Kawe jijini Dar es Salaam, kabla ya wahalifu hao hawajatekeleza azma zao.

Habari zaidi zinaeleza kwamba kuna baadhi ya nyaraka zimeibwa kutoka kwenye ofisi hizo na watu wasiojulikana, ambapo mpaka sasa ulinzi umeimarishwa eneo hilo, huku maafisa usalama, polisi waliovalia sare na waliovalia kiraia wakiendelea kuhakikisha amani inakuwepo eneo hilo.

Muonekano wa mbele wa ofisi hizo huku moto ukiendelea kuwaka.
Muonekano wa ndani wa ofisi hizo.

Leave a Comment