×

Ligi Kuu Bara…. Chunga Sana Hizi Sura

Tshimbi.

BAADA ya kusi­mama kwa zaidi ya miezi mitatu, ha­timaye uhondo wa Ligi Kuu Bara umerejea.

Mabingwa wa msimu uliopita, Yanga, watakuwa wakipambana kulitwaa taji hili mara ya nne mfu­lulizo, wakati timu nyingi zinaonekana kufanya usa­jili mzuri ambao ulithibitishwa na mechi za wikiendi iliyopita, kwa jinsi zilivyokuwa na msi­simko mkubwa.

Championi Ju­matatu linaku­letea timu ambazo zinaonekana zi­tasumbua vikali msimu huu na ku­chuana katika na­fasi za juu.

Niyonzima.

AZAM FC

Wengi wanawad­harau kwa kuwa hawajafanya usajili wa kutisha. Lakini niionavyo Azam, naamini itawaum­bua wengi. Imeon­dokewa na wache­zaji nyota kadhaa wakiwemo Erasto Nyoni, Aishi Manula na John Boc­co waliotua Simba pamoja na Gadiel Michael aliyetua Yanga lakini bado ina vijana wengi wenye vipaji pamoja na wakongwe.

Imefanya maandalizi mazuri. Ukiangalia mechi zake za kirafiki, imeshinda nyingi, na ndiyo timu iliyo­cheza mechi nyingi zaidi za kimataifa za kirafiki kuliko nyingine.

Mechi za kirafiki walizo­cheza Rwanda na baadaye Uganda, zitakuwa zime­wapa somo kubwa. Mechi nyingi za kirafiki, zimem­fanya kocha Aristica Cioaba kutambua kikosi chake cha kwanza tofauti na wap­inzani wake wengi, pia hata wachezaji wenyewe wametambuana vizuri.

Okwi.

MBEYA CITY

Itakumbukwa msimu uliopita ilipozika­zia timu kubwa za Simba na Yanga. Ingawa makali yake yamepun­gua tofauti na ili­vyopanda ligi kuu miaka kadhaa ili­yopita na kushi­ka nafasi ya tatu, bado naiona ni timu sumbufu, licha ya kuon­dokewa pia na wachezaji wake kadhaa muhimu.

Ina wache­zaji kad­haa wenye uzoefu wak­iwemo Mrisho Ngassa, Haruna Shamte na Has­san Mwasapili.

Bado ina mgogoro na kocha wake Mzam­bia, Kinnah Phiri lakini na­tarajia kuiona ikichuana katika nafasi za juu.

Chirwa.

SINGIDA UNITED

Japo imepanda daraja msimu huu lakini kwa usa­jili ilioufanya pamoja na ud­hamini mkubwa ili­onao wa kam­puni ya kubashiri matokeo ya SportPesa, naiona ikiwa haimuachi mtu salama.

Nguvu nyingine kubwa iliyonayo ni kocha mzoefu Hans van Der Pluijm aliye­wahi kuinoa Yanga. Lakini kikubwa imefanya usajili wa kutisha kuliko timu ny­ingine zote ndo­go na imefanya maandalizi mazuri.

Ngasa.

YANGA

Awali wengi wa lionekana kuibeza Yanga kutokana na kua­mini msimu huu haijasa­jili vizuri, hasa baada ya kuondoka kwa Haruna Niyonzima na Simon Msuva, lakini il­iwaum­bua wengi Juma ­tano iliyopita katika mchezo wa Ngao ya Jamii pale ilipoipe­lekesha Simba licha ya kufungwa kwa penalti.

Yanga kwa asilimia kubwa ni kikosi kilekile kili­chotwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara mara tatu mfululizo, lakini imejibore­sha sana kwa kum­sajili Mcongo, Papy Kabamba Tshishimbi na Ibrahim Ajibu kutoka Simba. Kwa hiyo, imekuwa safu pana na imara ya ush­ambuliaji ikiwa pia na masu­pastaa Donald Ngoma, Amis­si Tambwe na Obrey Chirwa.

Kombinesheni ya Tsh­ishimbi, Thaban Kamusoko na kiungo mwingine mpya Rafael Daudi, inaonekana itasumbua vilivyo kwenye ligi, hasa katika kiungo.

Baadhi ya mashabiki wa­nadhani Yanga hii ni dhaifu sana, wakiilinganisha na Sim­ba kwa usajili waliofanya la­kini nikwambie tu kuwa kwa mtazamo wangu, hakuna timu itakayokuja kufanya vye­ma kama Yanga, kwani Simba wamesajili wachezaji bila ya kuangalia wapi kulitakiwa kuzibwa gepu. Tatizo pekee linaloweza kuwaondoa relini labda ni ukata, kwa kuwa in­aonekana hawana vyanzo vya uhakika vya mapato.

SIMBA SC

Hawa jamaa safari hii wa­metisha kutokana na kuwa na kikosi kipana na chenye maji­na makubwa ya wachezaji, la­kini siku zote kujiamini kwingi kuna madhara makubwa.

“Mpira ni tofauti na draft, ukikutana na anayejua basi jua utapigwa supa lakini to­fauti na mpira wa miguu un­aweza ukawa unajua lakini ukafungwa,” kauli hii aliitoa msemaji wa Simba, Haji Man­ara, kikosi chao cha bil 1.3 kime­kuwa tishio kubwa msimu huu kwani kimeanza vye­ma maandalizi yake.

Kwa usajili waliofanya na jinsi timu hiyo ilivyo na hamu ya kuchukua ubingwa wa ligi kuu msimu huu moto wataka­ouwasha siyo wa kitoto.

Sasa ina wachezaji wengi wazoefu, mfano Emmanuel Okwi, John Boc­co, Niyonzima, Shiza Kichuya, Aishi Manula, Erasto Nyoni, Shomari Ka­pombe pamoja na wenye vipaji kama Moham­med Ibrahim, Mzamiru Yassin na wengine. Wanahitaji kuzoeana tu waanze kufan­ya yao.

KAGERA

Timu hii ipo kimya lakini moto wake ni kama wa kifuu, huwa unawakia ndani kwa nda­ni. Msimu ulio­pita walimaliza nafasi ya tatu na kocha wao Mecky Maxime akachukuwa tuzo ya kocha bora.

Msimu ulio­pita walimaliza nafasi ya tatu chini ya Simba na Yanga, ukia­chana na usa­jili wao mdogo waliofanya la­kini kocha wao Maxime ndiyo mpango mzi­ma. Mara zote hutoa ushinda­ni mkubwa, tan­gu alipokuwa Mtibwa.

Ibrahim Mressy, Dar es Salaam

Leave a Comment