
Prodyuza aliyewahi kumtengenezea ‘hit songs’ kibao mwanamuziki Barnaba Classic, kama vile Lover Boy, Tunafanana na nyingine nyingi, D Classic, amefungukia mkataba wake na mwanamuziki huyo, kuwa haumfungi kuwa na rekodi lebo yake na kumiliki wasanii wake, kama anavyofanya sasa kwa rapa mkali na chipukizi, Rasco.
“Watu wengi wanahisi kwamba, nina mkataba na Barnaba ambao unanifunga kufanya kazi zangu binafsi za muziki, kitu ambacho siyo kweli, ninafanya naye kazi pale tu inapotokea kuna kazi.

“Sasa hivi nina rekodi lebo yangu inaitwa I Deal One Entertainment ina msanii mmoja anaitwa Rasco, ambaye tayari ameachia ngoma inayoitwa Choro aliyomshirikisha Coyo, ila bado ana ngoma nyingi sana ambazo tutaziachia hivi karibuni,” alisema D Classic.
NA ISRI MOHAMED/GPL