×

Majimaji: Sokabet Imetupa Nguvu, Yanga Kazi Wanayo!

Mwenyekiti wa Klabu ya Majimaji, Steven Ngonyani (kulia) na Mratibu wa Sokabet, Franco Ruhinda wakisaini mkataba wa kuidhamini Majimaji.

SOKA la sasa ni bi­ashara, klabu nyingi zimekuwa zikipata nguvu kubwa kutoka­na na udhamini, hivyo ndivyo inavyoonekana kwa Klabu ya Majimaji ambayo ni moja ya klabu kongwe nchini, baada ya kupata udhamini wa mwaka mmoja wa Kampuni ya Sokabet.

Mastaa wa Soka, Bongo Movie Waifungukia Sokabet

Kampuni hiyo inayojihusisha na michezo ya kubashiri matokeo, imeonyesha dalili za kuipa nguvu Majimaji ambapo tayari mwitikio wake ndani na nje ya klabu hiyo ni mkubwa.

Kabla ya udhamini huo, Ma­jimaji ilikuwa ikionekana kuto­kuwa vizuri kiuchumi, kuthibitisha hilo ni jinsi ilivyo safari ya usiku mnene kutoka Songea kuelekea Mbeya kwa basi na kuingia Mbeya asubuhi ya siku ya mchezo wao dhidi ya Mbeya City, hivi karibuni.

Mwenyekiti wa Klabu ya Majimaji, Steven Ngonyani.

Katika mchezo huo wa Ligi Kuu Bara, Majimaji ilipoteza kwa ku­fungwa bao 1-0, lakini kabla ya kucheza mchezo uliofuata dhidi

ya Prisons, Majimaji ilipata bahati ya kusaini mkataba na Sokabet wenye thamani ya Sh milioni 150.

Kwenye mchezo dhidi ya Prisons, Majimaji iliwasili Mbeya mapema na ilifanikiwa kutoka sare ya bao 2-2 huku wachezaji wake wakicheza vi­zuri kwa asilimia kubwa. Mch­ezo unaofuata wikiendi hii itakumbana na Yanga katika kipute kitakachopigwa kwenye Uwanja wa Majimaji, Songea.

Leo Jumamosi, Majimaji itaivaa Yanga na inaelezwa kuwa wapo fiti na tayari kwa ajili ya mchezo huo wa Ligi Kuu Bara, je, unafahamu ni kwa namna gani Sokabet wame­pokewa Songea? Ifuatayo ni mitazamo ya Wanalizombe hao:

Mtangazaji wa Azam akifanya mahojiano na mchezji wa Majimaji.

OFISA HABARI WA MA­JIMAJI

“Wazungu wanasema some­thing is better than nothing, kwa maana ya bora kupata ki­dogo kuliko kukosa kabisa, sisi tumewapokea Sokabet kwa fu­raha kubwa mno, na tutafanya nao kazi vizuri kwa manufaa yetu sote.

“Sokabet wametuokoa kwenye kipengele cha misha­hara, viongozi tunajipanga ili kuhakikisha tunaweka maz­ingira rafiki ya kufikisha jezi zenye nembo ya Sokabet kwa mashabiki wetu,” anafafanua Ofisa Habari wa Majimaji, Onesmo Ndunguru.

MENEJA WA MAJIMAJI

“Wachezaji wetu baada ya kusikia tumepata ufadhili huu wamezidisha juhudi za kupambana uwanjani, tunaku­tana na Yanga kikosi chetu kikiwa vizuri kisaikolojia na kifiziki naamini tutaibuka na ushindi.

“Pia tunaomba msimu ujao wasituache kwa kuwa ud­hamini wao ni muhimu sana kwetu,” anafa­fanua Godfrey Mvula ambaye mwaka huu ametimiza miaka 17 ya umeneja ndani ya timu hiyo.

KOCHA WA TIMU

“Ni udhamini mzuri, tunashukuru wametu­unga mkono. Viongozi waen­delee kutafuta wadhamini wengine ili tunufaike zaidi,” anasema Peter Mhina, kaimu kocha mkuu.

Sokabet… Shinda Milioni 100

WACHEZAJI

“Sisi kwa upande wetu tu­me furahia sana na kama ina­vyofahamika mpira wa siku hizi ni fedha. Majimaji mara nyingi inafanya vibaya kwa ku­kosa fedha. Udhamini wao utatusaidia sana,” anasema Danny Mrwanda am­baye ni nahodha wa timu hiyo.

Akizungumzia juu ya ud­hamini huo, Mratibu wa Soka­bet, Franco Ruhinda anasema mipango ya kampuni yao ni kukuza mchezo wa soka na mingine, kwa kuanzia wamean­za na Majimaji lakini baada ya hapo mipango yao ni mikubwa katika jamii ya Tanzania, am­bapo udhamini huo ni kureje­sha kwenye jamii kile ambacho w a t a k u w a w a k i k i p a ­ta katika michezo ya kubashi r i matokeo.

A i d h a , F r a n c o a l i o n g e z a kuwa wale wanaotaka ku­bashiri matokeo wanaweza kufanya hivyo kwa kufungua tovuti ya www.soka­bet.co.tz ambapo kwa kutumia namba ya kampuni ya 335757 wanaweza kuingiza fedha kwenye akaunti zao na kubet.

Anafafanua zaidi kwa kuse­ma, baada ya kufungua akaun­ti mtumiaji anaweza kuingiza fedha kisha kuanza kubeti.

Anasema kwa watumiaji wa Vo­d a ­com wanaweza kuingiza salio kwa kub­onyeza *150*00#, chagua namba 4 (lipa kwa M-pesa), chagua namba 4 (weka namba ya kampuni), ingiza namba ya kampuni am­bayo ni 335757, kisha ingiza kumbukumbu ambayo ni neno ‘Sokabet’.

Baada ya hapo ingiza kiasi unachotaka mfano Sh 1,000 au 5,000 na kuende­lea, utamalizia kwa kuin­giza namba yako ya siri na bonyeza namba 1 kukamili­sha mchakato.

Kwa Tigopesa, bonyeza *150*01#, chagua namba 4 (lipia bili), bonyeza namba 3 (ingiza namba ya kampuni), ingiza namba 335757, kisha ingiza kiasi cha fedha, in­giza neno ‘Sokabet’, malizia na namba yako ya siri ya Tigopesa.

Kwa Airtel bonyeza *150*60#, chagua namba 5 (lipia bili), bonyeza namba 4 (namba ya kampuni), ingiza namba 335757, kisha ingiza kiasi cha fedha, itakwambia ingiza kumbukumbu nam­ba (hapa ingiza neno ‘Soka­bet’), kisha namba yako ya siri ya Airtel money.

MAKALA, CHAMPIONI JUMAMOSI

Leave a Comment