
WAHARIRI wa Gazeti la MwanaHalisi linalomilikiwa na Mbunge, Saed Kubenea lililofungiwa na serikali wamekanusha taarifa ya serikali kuwa gazeti hilo linaandika habari za uongo, wamedai kuwa wao hawajawahi kuandika uongo na badala yake huandika habari kwa weledi na ukweli.
Hayo wameyasema leo jijini Dar es Salaam wakati wakizungumza na wanahabari baada ya gazeti lao kufungiwa kwa muda wa miezi 24 (miaka miwili). Amesema wamefikia uamuzi huo baada ya kubaini kuwepo na uonevu wakati wa kulifungia gazeti hilo.
Breaking News: Serikali Yalifungia Gazeti la MwanaHalisi
Aidha mmiliki wa Kampuni ya hali Halisi Publishers Ltd wachapishaji wa gazeti hilo, Saed Kubenea amesema kampuni yake imeiandikia barua Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakiitaka serikali kulifungulia Gazeti lao ndani ya siku mbili (jana na leo), na kusema kuwa endapo serikali ikikataa ombi lao watamfungulia kesi binafsi mahakamani Naibu Waziri wa Wizara hiyo aliyelifungia gazeti lao, Anastazia Wambura ya kumdai fidia ya milioni 141 kwa kila chapisho la gazeti ambalo litakuwa halitoki tangu kufungiwa kwa madai sheria haijampa mamlaka ya kulifungia gazeti.
“Tumewaandikia barua hawa watu kuwa ndani ya siku mbili walifungulie Gazeti hili,na kama wakikaidi mwanasheria yupo hapa tunakwenda kufungua kesi binafsi kwa Naibu waziri ,tunataka watulipe hela hii ya milioni 41 moja ya kila toleo la gazeti ambalo alitoki ikiwa ni hasara aliotuingizia,” amesema Kubenea.
Kubenea ambaye ni Mbunge wa Ubungo (Chadema) amesema hata hatua ya serikali kuliifungia gazeti la Mwanahalisi ni kuidharau muhimili wa mahakama kutokana na Mahakama kuu kutoa umuzi wa kutoguswa gazeti hilo.
“Leo tunashangaa serikali hii inapuuza uamuzi wa mahakama ambao ulitaka gazeti hili lisiguswe kwa namna yeyote,maana Jaji alisema kama waziri akitaka kuligusa gazeti hili anatakiwa kwenda mahakamani na mahakama kutoa maauzi,lakini tunashangaa leo wanakuja kulifungia gazeti”
“Na hata ukiangalia barua ya kufungia gazeti hili,imesainiwa na Naibu waziri wakati sheria ya Huduma ya habari ya 2016 imemtaja Waziri na sio naibu waziri,pia sheria hiyo haimpi waziri kulifungia gazeti bali inamtaka kuzuia tu maudhui sio kufungia gazeti,” amesema Kubenea.
Naye Mwanasheria wa Kampuni hiyo,Fredrick Kiwelo amesema kwa sasa wameshamwandikia notsi ya siku mbili Naibu waziri kuondoa zuia la kulifungia Gazeti.
“Hawa tumewashaaandikia barua,huku tujiandaa kwa taratibu zengine za kufungua kesi za kudai fidia maana kumetokea ukiukwaji mkubwa kwenye kulifungia kesi’Amesema Kiwelo.
KUHUSU TUHUMA ZA GAZETI LA MWANAHALISI
Kubenea ambaye ni Mwandishi Nguli wa habari nchini kwa sasa, amesikitishwa na maelezo yaliyotolewa na Mkurugenzi wa habari Maelezo,Dkt Hassan Abasi kuwa gazeti la mwanahalisi limekuwa likiandika habari za kutunga na zenye kukiuka kanuzi na misingi ya taaluma na habari.
Kubenea amesema maelezo ya Mkurugenzi huyu ni ya kupuuzwa kwani gazeti lake limekuwa likiandika habari za ukweli.
“Hili Gazeti linaendeshwa na watu weledi kwenye vyombo vya habari si vyeti tu bali wanauadilifu mkubwa wa kimaadili,leo miongoni mwa wahariri wa gazeti hili ni, Nyaronyo Kichele huyu alikuwa ni mhariri wa gazeti la Kulikoni ambalo hapa Abassi ndipo alipofanya kazi,sasa leo walimfundisha kazi huyu Abassi leo ndio wanaandika habari za uongo?” Amehoji Kubenea.
Mbunge huyu Mchachali amesema kwa sasa kinachoisumbua serikali kwa sasa ni kutokana na wamiliki wa gazeti hilo kukataa “kuilamba miguu serikali”
“Nataka ni waambieni tulipofungia mara ya kwanza mwaka 2012 kutokana na kuandika habari ya kutekwa,kupigwa na kutupwa kwa kiongozi wa madaktri nchini Dk Steven Ulimboka,tulimtaja mtu mmoja anaitwa Ramadhan Igondu kuwa nahusika ,na hata serikali hakuna mahala popote walipokanusha kuhusu huyu mtu na hata Dk Ulimboka alikuja na kukiri kumfahamu huyu mtu na akamtaja nahusika,”
“Na hata tulipokwenda mahakamani serikali ikatufungulia gazeti ,sasa leo unaposema gazeti hili linaandika habari za uongo ni vipi”ameendelea kuhoji.
Hii imekuja ikiwa ni wiki moja tangu serikali kulifungia kwa mwaka miaka miwili gazeti la Mwanahalisi, kwa madai ya kuwa Gazeti hilo linaandika habari zinazokiuka kanuni za uandishi wa habari,Wamiliki Gazeti hilo wameibuka na kuipa siku mbili serikali kulifungulia gazeti hilo kabla ya kwenda mahakamani.