×

Takwimu Zinaonyesha ni Mechi Ya Ajibu na Okwi

Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi.

UTAMU wa tak­wimu kwa mchezaji una­tokana na anavyojitu­ma kusaidia jambo fu­lani hasa unapokuwa kiungo timu yako inacheza vizuri na kushinda au msham­bulizi unayefunga ma­bao na kusaidia kuzal­isha pointi.

 

Inawezekana pia ukawa mlinzi au kipa na kusaidia timu kuto­fungwa au kufungwa mabao machache. Zote hizi zi­naingia katika takwimu.

Wache­zaji wawili, Ibrahim Ajibu wa Yanga na Emmanuel Okwi ndiyo wanachochea watu 23,000 wanaoweza kuingia kwenye Uwanja wa Uhuru, wajikute wa­nashawishika zaidi ku­fanya hivyo.

 

Simba itakuwa ina­ivaa Yanga kwenye uwanja huo Jumamosi lakini gumzo limekuwa hao wawili na wanacho­tarajiwa kukifanya.

Yanga walikosa matu­maini, hawakuwa na mtu wa kuwatishia watani wao kwa kuwa Amissi Tambwe na Donald Ngoma wanasum­buliwa na majeraha wakati Obrey Chirwa ndiyo anaanza kurejea lakini walikuwa na hofu kubwa na Emmanuel Okwi, pia Shiza Kichuya.

Mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajibu.

Lakini sasa, wakati Chirwa anarejea huku kukiwa na matarajio ya kuwaona Ngo­ma na Tambwe, anayebeba matumaini ya mioyo yao ni Ajibu ambaye amejiunga na Yanga akitokea Simba.

 

Takwimu za ndani zi­naonyesha Ajibu kweli ni bora na tangu atue Yanga ameachana na “utoto” na sasa anapiga kazi na kweli inaoneka­na na Simba wana hofu h a s a kukutana na “kija­na” wao m a a n a a n a fan­ya kazi yake.

O k w i na Ajibu wa­naweza wakawa hawafanani sana kiuchezaji lakini majibu ya takwimu zao kwa wana­chokifanya yanawafanya waonekane ni wa aina moja na wanaowapeleka watu uwanjani au kuwafanya wakae wakiangalia runinga.

 

Swali, Okwi au Ajibu watafanya nini, nani atafanya vizuri zaidi au yupi ataanza kufunga?

Kwa kasi w a l i y o n a y o wana nafasi ya kufanya vizuri kwa kufunga au kutengeneza nafasi ya kufunga. Lakini watataki­wa kutulia na kuwekeza akili zao, la sivyo mpira utawashinda kutokana na presha kubwa kuan­gushiwa vifuani mwao.

TAKWIMU ZAO:

MABAO:

OKWI:

Okwi ana mabao nane, matatu zaidi ya Ajibu akiwa amecheza dakika pungufu na hii inam­fanya awe hatari zaidi kwa maana ya kuwa ana uwezo mkubwa zaidi wa kufunga licha ya kucheza dakika chache.

Okwi amecheza dakika 493 na Ajibu amecheza dakika 610.

AJIBU:

Ajibu ana mabao matano, lakini ame­onyesha ni mwiba kwa kuwa mabao yake mengi hautarajii. Ni mchezaji ambaye atawapa wakati mgumu kumkaba na kwa kuwa angetaka kutimiza furaha yake kuifunga Simba, basi ataongeza juhudi na umakini.

UHURU:

OKWI:

Uwanja wa Uhuru ni kama nyum­bani kuliko Ajibu kwa kuwa ame­funga mabao yote nane katika uwanja huo. Inam­p a n a ­f a s i y a kujiamini zaidi.

AJIBU:

Ajibu amefunga kwenye uwanja huo likiwemo bao zuri dhidi ya Ndan­da FC. Lakini hiyo haimzuii kufunga au haimpi uhakika wa kufunga.

Ukiachana na bao lake dhidi ya Ndanda kwenye uwanja huo, Ajibu amefunga mabao dhidi ya Kagera Sugar-Kaitaba, dhidi ya Stand United akapiga mawili pale Kambarage.

Lakini kum­buka alifunga bao la mkwaju wa adhabu Yanga ikiwa ugenini dhidi ya Njombe Mji.

KICHWA:

OKWI:

Amefunga mabao mawili ya kichwa, hii i n amf a n y a kuwa na na­fasi kubwa zaidi ya k u f u n g a k a m a Simba watatu­mia mipira ya krosi ingawa wana wapiga vichwa wazuri kama Kelvin Yonda­ni na Nadir Haroub au An­drew Vincent.

AJIBU:

Hajafunga bao lolote la kichwa zaidi ya kuonyesha mguu wake wa kulia ni hatari sana. Kama haujajua, Ajibu ana uwezo mkubwa wa kupiga mashuti akipata nafasi na mfano ni bao lake la pili dhidi ya Stand.

KUJENGA:

OKWI:

Wanasema nafa­si zinatengenezwa lakini unaweza kuz­ijenga vizuri kupi­tia timu au mtu. Okwi ana uwezo wa kutengeneza nafasi akiwa ana­kimbia na mpira na mkimuachia nafasi anaachia mkwaju na kufunga, katika mabao nane aliyo­funga, mawili ame­fanya hivyo.

AJIBU:

Ajibu hakim­bii sana na mpira, tofauti yake na Okwi anaweza ku­wapita mabeki akiwa katika kasi. Ajibu ana uwezo wa kumuacha beki wakiwa wamesima­ma, akatoa pasi na kuchukua nafasi, yaani ni mzuri wa kutafuta nafasi na anaweza kuibore­sha na mara ny­ingi hufanya hivyo wakati anapokea mpira.

Pasi aliyopewa na Chirwa ka­tika mechi dhidi ya Stand, mpira alikuwa kama ameutuliza lakini tayari alishauinua kidogo kumpa na­fasi ya kupiga shuti analotaka lakini alishampoteza beki aliyekuwa karibu yake.

FAULO:

Okwi na Ajibu wote ni hatari sana wana­pokuwa nje na ndani ya eneo la 18, ni rahisi sana k u s a b a b i ­sha faulo kwa kuwa ni wepe­si na si waoga kupita katikati ya msimu wa ma­beki.

Mabeki wa kila upande wa­napaswa kuwa makini na kama watajisahau kwa kusababisha fau­lo, pia ni kuwa­tengenezea nafa­si.

Leave a Comment