×

Washindi 10 wa Vipaji vya Sauti StarTimes Wapatikana, Sasa Kupelekwa China

Coletha Raymond (kushoto) na mshiriki mwenzake wakiwa kwenye usaili.

USIKU  wa kuamkia leo, Shindano linalodhaminiwa na kampuni ya Star Media (T) Ltd kupitia StarTimes na chaneli yake ya Star Swahili lilifikia mwisho huku washindi 10 wakiibuka kidedea katika mchakatio wa kuwasaka machampioni hao

Msanii Pipi (kushoto) na mshiriki mwenzake wakiwa kwenye usaili.

Miongoni mwa watu walioibuka washindi ni Msanii wa filamu Bongo, Koletha Raymond, aliyeibuka mshindi namba moja baada ya kuwabwaga washiriki zaidi ya 25, aliyokuwa akichuana nao kwa ajili ya kuwania nafasi ya kwenda kufanya kazi makao makuu ya Kampuni ya Star Times, nchini China kuigiza sauti ya filamu mbalimbali zilizochezwa kwa lugha mbalimbali.

Majaji wakiwa makini kutoa alama kwa washiriki.

Shindano hilo lililofanyika usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa LAPF lililopo Millenium Tower Kijitonyama jijini Dar es Salaam, ambapo washindi 10, wataungana na Koleta kwenda nchini humo kwa ajili ya kufanya kazi hiyo ambayo wataifanya kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Mshindi akikabidhiwa zawadi yake ya flat screen.

Washindi hao wamepatikana katika ushindani mkali mbele ya majaji watatu wakiongozwa na wasanii Jacob Steven ‘JB’ na Mrisho Mpoto ‘Mjomba’ ambapo haikuwa kazi rahisi kwa majaji hao na washiriki wenyewe kutokana na ushindani mkali uliojitokeza.

Coletha akikabidhiwa zawadi ya flat screen.
Washiriki 25, watano kutoka Mwanza, watano kutoka Zanzibar na 15 wa Dar es Salaam, walichuana vikali kupata washindi 10 wanaokwenda kufanya kazi hiyo nchini China.
Washindi wote wakiwa na zawadi zao.

Mmoja wa waigizaji maarufu nchini, Muhogo Mchungu alijikuta akiangukia pua baada ya kuzidiwa ujuzi na vijana.

Jaji, JB akimpongeza Coletha.
Balozi wa China  nchini Tanzania akiwapongeza washindi.
Washindi katika picha ya pamoja.
Kutoka kushoto ni mshindi wa kwanza hadi wa tatu.
Washindi wakifurahia.

Musa Mateja | Glob al Publishers

SHUHUDIA LIVE: Birthday ya Aunty Ezekiel, Masaki Dar ni Kufuru

Leave a Comment