
LIGI Kuu ya Hispania, La Liga, inaendelea kutikisa huku kila timu ikionyesha kiwango cha hali ya juu uwanjani.
Wikiendi iliyopita haikuwa mbaya sana kwa kuwa timu nyingi vigogo ziliendelea kupata ushindi jambo ambalo liliifanya ligi hiyo kuendelea na utawala uleule.
Barcelona tayari wamejijengea miliki kwenye ligi hiyo wakiwa kileleni kwa sasa tofauti ya pointi nne dhidi ya Valencia ambao wanashika nafasi ya pili.
Lakini ajabu ni k w a m b a pamoja na Real Madrid kuibuka na ushindi kwenye mchezo wake wa wikiendi, Barcelona imewaacha kwa pointi nane, jambo ambalo linaonekana kuwa gumu sana kwao kuamini kuwa wanaweza kufanya vizuri msimu huu.
Staa wa Barcelona, Lionel Messi ameendelea kutawala kwenye chati ya ufungaji kwenye ligi hiyo na Ulaya kwa ujumla baada ya kufanikiwa kufunga mabao 12, hadi sasa kwenye ligi huku akiwa hana upinzani mkubwa kutokana na Cristiano Ronaldo ambaye amekuwa akifanya vizuri kwa miaka kadhaa iliyopita kupotea na hadi sasa ana mabao mawili tu kwenye ligi hiyo.

L a Liga ya msimu huu imeonekana k u w a tofauti kidogo k u t o k a n a na hadi sasa timu tatu kuwa hazijap o t e z a mchezo wowo t e jamb o amb a l o limekuwa halitok e i k w e n y e ligi hiyo misimu mingi iliyopita.
Hali hii inaonyesha kuwa upinzani kwa sasa umeongezeka kwenye ligi hiyo, kwa kuwa pia timu nyingi ambazo zilikuwa hazipewi nafasi ya kuwika ndizo zimeonekana kuchukua nafasi mbili za juu.
Timu ya Barcelona haijapoteza mchezo wowote, lakini ajabu ni kwamba inalingana na Atletico Madrid pamoja na Valencia, ambazo zote zimeshacheza michezo 11 bila kupoteza.

Wachambuzi wa masuala ya soka la Hispania wanaamini kuwa kuna uwezekano mkubwa kukawa na mabadiliko kwenye msimamo wa ligi hiyo mwishoni mwa msimu huu tofauti na hali ilivyokuwa misimu iliyopita.
Hii ni mara ya k w a n z a k weny e l i g i h i y o t i m u kucheza m i c h e z o mingi namna hiyo bila k u f u n g w a hata mmoja ndani ya miaka 20 iliyopita.
W e n g i wana amini k u w a kuna mab a d i l i k o makubwa j a m b o a m b a l o limechangia Madrid kuonekana kuwa chini kwa sasa tofauti na hali ilivyokuwa hapo nyuma.
Barcelona wenyewe tayari wameshatishia kwenye ligi hiyo wakiwa wameshinda michezo nane na kutoka sare michezo mitatu na ndiyo timu inayopewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri kwa msimu huu.
Hata hivyo, kwa Atletico wenyewe hili siyo jambo la ajabu kwa kuwa ni mara ya tatu kwa sasa wanacheza michezo 11 bila kufungwa, walifanya hivyo msimu wa 1996/97 na 1982/83.
Mara ya mwisho kwa ligi hiyo kuwa na timu tatu ambazo hazijafungwa baada ya michezo 11 ilikuwa msimu wa 1996/97, wakati Barcelona, Real Madrid na Deportivo zilipocheza michezo 12.
“Hatuna presha kubwa, hili ni jambo la kawaida na linaweza kutokea, sisi kukosekana kwenye timu hizo tatu ni mabadiliko ya ligi na wala siyo kitu kinachoweza kutusumbua sana.
“Ni vizuri kwa kuwa tunafanya vitu vyetu kwa mpangilio mzuri na tunaamini kuwa mwisho wa msimu ndiyo kila kitu kitakuwa wazi,” alisema beki na nahodha wa Real Madrid, Sergio Ramos.
Hofu kubwa ipo kwa Madrid ambao kwenye michezo hiyo 11 wameshapoteza miwili lakini wakiwa na sare mbili matokeo ambayo siyo mazuri sana kwao kwa msimu huu.