
Pamoja na juhudi kubwa za Klabu ya Simba kufanya juhudi za kumficha kocha wake mpya Mfaransa, Gazeti la CHAMPIONI limefanikiwa kumuibua mafichoni.
Kocha huyo anayejulikana kwa jina la Mfaransa Pierre Lechantre alitua nchini juzi Jumanne, januri 16, 2017 usiku na uongozi wa Simba umefanikiwa kumficha hadi alipoibuliwa na gazeti hilo na anatarajia kusaini mkataba na Simba leo.
Lechantre amekuja pia na kocha wa viungo Mmorocco Mohammed Aymen Hbibi ambapo ataanza kazi mara moja na akisaidiwa na kocha msaidizi wa sasa Masoud Djuma ambae alikuwa akikaimu nafasi hiyo.
Kocha Lichantre keshawahi kufundisha klabu kadhaa duniani kikiwemo kikosi cha Timu ya Taifa ya Cameroun kilichotwaa ubingwa wa Africa 2000.
Kocha huyo pia alipata kuwa kocha bora wa Afrika mwaka 2001 na pia barani Asia mwaka 2012.
TAARIFA KWA UMMA
Klabu ya Simba inayo furaha kubwa kuwajulisha wanachama na mashabiki wake kwamba imempata kocha wake Mkuu mpya, Mfaransa Pierre Lechantre. pic.twitter.com/v8GdChnB7w
— Simba SC Tanzania (@SimbaSCTanzania) January 18, 2018