×

Hakuna Anayemuweza Dude Zaidi ya Mkewe

KIDUME wa Bongo Movies, Kulwa Kikumba ‘Dude’ amenyoosha sentensi kuwa, hakuna mwanamke anayemuweza kuishi naye zaidi ya mkewe, Eva kwani ni mwanamke mvumilivu kuliko yeyote chini ya jua.

 

Dude aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa, kuna wakati anafikiria mno kuwa ni zawadi gani anayoweza kumpa ili iwe sawa na thamani ya vitu alivyomfanyia kwani kama ni kumkosea, ameshamkosea mara ‘kibwena’, lakini bado anaendelea kumuonesha mapenzi yaleyale.

 

“Niamini mimi, hakuna mwanamke anayeweza kuishi na mimi, lakini kwa mke wangu ameshinda mitihani yote hadi kuna wakati ninajishtukia mwenyewe,” alisema Dude na kuongeza kuwa, Eva anajua kulea familia vyema kama mama mwenye kuwafundisha watoto wake maadili mema.

Stori: Imelda Mtema, Dar