Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli, amemwapisha Dkt. Adelardus Kilangi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Paul Ngwembe, kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Sherehe za kuapishwa kwa Kilangi na naibu wake, zimefanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, ambapo Rais Magufuli pia amemwapisha aliyekuwa Mwanasheria Mkuu, George Masaju na aliyekuwa naibu wake, Gerson Mdemu kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.
Kabla ya uteuzi, Dkt. Kilangi alikuwa Mkurugenzi wa chuo kikuu cha Mtakatifu Augustino Kituo cha Arusha na pia mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa juu wa mafuta.
Naibu Mwanasheria mkuu, Paul Ngwembe kabla ya uteuzi, alikuwa mkurugenzi wa masuala ya sheria katika mamlaka ya usimamizi wa bima Tanzania.