
Mwili wa marehemu Akwilina Akwilini umeagwa leo Feb 22, 2018 katika viwanja vya Chuo cha NIT kabla ya kusafirishwa kwenda Rombo kuzikwa.
Zoezi la kuaga mwili wa Akwilina limeongozwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Mkuu wa Chuo cha NIT, Prof. Zacharia Mganilwa, ndugu wa marehemu, wanafunzi wenzake, marafiki na Wananchi kutoka sehemu mbalimbali za nchi walifika kumuaga binti huyo.

Global Publishers na Global TV Online inatoa pole kwa ndugu, marafiki, wanafunzi wa NIT na wote walioguswa na msiba wa Akwilina.

Mwenyezi Mungu ailaze mahali pema peponi roho yua marehemu. AMEN!






PICHA NA RICHARD BUKOS