
AJALI mbaya imetokea neo la Tabata TOT jijini Dar es Salaam,usiku wa kuamkia leo baada ya gari dogo lenye namba za usajili T222 DJX kugongana na lori la mizigo lenye namba za usajili T 495 na kuingia katikati na kubanwa na lori la mafuta lenye namba za usajili T 748 BMT.
Katika ajali hiyo, Mwandishi wa habari wa Gazeti la Uhuru, Mariam Mziwanda, aliyekuwa akiendesha gari hilo dogo amejeruhiwa na amedai kuumia kifuani, kichwani na mguu wa kulia.

Dereva wa lori la mafuta lililohusika katika ajali, William Colonel ameeleza kuwa, chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa lori la mzigo ambalo liliacha njia na kupanda kingo za katikati ya barabara, kisha kupinduka na kuangukia lori la mafuta na gari lililokuwa likiendeshwa na Mziwanda.
Aidha, madereva wote wa malori walitoka salama bila majeraha ya aina yoyote.