×

TFF ya Misri Yawabeba Al Masry

KATIKA kuhakikisha timu ya Al Masry inafanya vyema kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Chama cha Soka cha Misri (EFA), kimepangua ratiba yake na kusogeza mbele mchezo kati ya Al Ahly dhidi ya Al Masry.

Sababu kubwa ya uamuzi huo ni kutokana na Al Masry kukabiliwa na mchezo dhidi ya Simba ambao utapigwa hapa jijini Dar es Salaam, Machi 7, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa.

Mchezo huo ulitakiwa kupigwa keshokutwa Jumapili ya Machi 4, mwaka huu katika mwendelezo wa Ligi Kuu ya Misri.

Al Masry ambao wapo nafasi ya nne kwenye ligi hiyo, wamecheza michezo 26 wakiwa na pointi 45 ambazo ni sawa na wapinzani wao Simba walio na alama hizo baada ya kucheza michezo 19.

Aidha, leo Ijumaa, Al Masry itacheza dhidi ya Alassiouty huku Simba ikicheza na Stand United kwenye Uwanja wa Taifa.