×

FT: YANGA 1-2 TOWNSHIP ROLLERS, CAF CHAMPIONS LEAGUE

MPIRA UMEKWISHA

Dak ya 92, Dakika 3 ziliongezwa, sekunde kadhaa sasa mpira uishe

Dak ya 88, Mwashiuya anapiga kona lakini mpira unatoka nje, ni goli kiki

Dak ya 83, Goooooli Rollers wanapata bao la pili

Dak ya 77, Mwashiuya anapiga kona kuelekea lango la Rollers, ni kona ya 8 kwa Yanga, anapiga lakini mabeki wa Rollers wanaokoa

Dak ya 73, Yanga wanapasiana nyuma, Kabwili anao, anapiga mbele unaendaaa mpaka kwa kipa wa Rollars

Dak ya 71 Obrey Chirwa anapigwa kadi ya njano

Dak ya 68, Ameingia Mwashiuya kuchukua nafasi ya Ajibu

Dak ya 64, Hassan Kessy anapewa kadi ya njano baada ya kucheza madhambi, Mwashiuya anapasha nje ya dimba

Dak ya 61, Matokeo bado ni 1-1

Dak ya 59, Inapigwa krosi kali langoni mwa Yanga, inapigwa kichwa na mshambuliaji lakini inadunda chini na kupaa juu ya nyavu za Yanga, ilikuwa hatari

Dak ya 54, Yanga wanapata kona, inapigwaaa, lakini mabeki wanaokoa, Tshishimbi anauchukua tena apige lakini mpira unakwenda nje

Dak ya 53, Yanga wanapasiana eneo la kati mwa uwanja

Dak 45 zimekamilika, matokeo ni 1-1.

Da ya 44, Ajibu anapiga faulo, huku mchezaji aliyeumia akitoka nje, anapiga, kipa anaokoa inagonga mwamba, Offside

Dak ya 42, Yanga wanapata free kiki kulia mwa uwanja karibu na eneo la hatari la Rollars

Dak ya 37, Rollers wanajaribu kupata bao lakini Yanga wanaokoa

Dak ya 32, Inapigwa tena, kunatokea hekaheka langoni kati ya kipa na mabeki lakini kipa anaudaka

Dak ya 30, Goooooooo, ni Chirwaa, sasa ni 1-, kazi nzuri ya Tshishimbi inaleta matunda

Dak ya 21, Yanga wanapata kona, anapiga lakini Chirwa anashindwa kuumudu, unatoka nje

Dak ya 20, Yanga 0-1 Township, Yanga wanashambulia kwa kasi kutafuta bao

Dak ya 19, Chirwa sasa anakimbiza na kumuwekea Buswita lakini mabeki wanaokoa

Dak ya 17, Matokeo bado ni 1-0, Township wanaongoza, kipa Rostand anapasha, inawezekana aakachukua nafasi ya Kabwili

Dak ya 15, Hatariiii, linapigwa shuti kali na mshambuliaji wa Township lakini linagonga mwamba, ni hatari

Dak ya 11, Rollers wanaanza tena taratibu, Yanga wanauchukua, beki Isubo wa Rollers anaokoa

Dak ya 10, Goooooo, Rollers wanapata bao la kwanza

Dak ya 10, Makapu anaokoa mpira uliopigwa langoni wa Yanga, Rollers wanauchukua tena na sasa wanapasiana eneo la hatari la Yanga.

Dak ya 9, Faulo inapigwa kuelekea lango la Yanga baada ya Sisikele kuchezewa faulo

Dak ya 8, Kessy anapasiana na Papy, Papy anampa tena Kessy, Kessy anapoteza wanachukua Township

Dak ya 6 Timu zinashambuliana kwa zamu

Dak  ya 3, Hatari, mshambuliaji wa Rollers anakosa bao la wazi hapa, matokeo ni 0-0

2′ Timu zote zinasomana.

Mchezo umeanza

Mgeni rasmi Waziri Mwakyembe anakagua vikosi vya timu zote mbili.

Mtanange wa Klabu Bingwa Afrika kati ya Yanga wakikipiga Township Rollers ya Botswana katika Dimba la Taifa jijini Dar es Salaam.