
MKE wa Rapa maarufu Bongo, Ibrahim Mussa ‘Roma Mkatoliki’, Nancy Mshana ‘Mama Ivan’ amefunguka kuwa mume wake kwa sasa anapitia katika wakati mgumu hasa kuhusu muziki wake na maisha yake kwa ujumla kiasi cha kutamani aache muziki.
Mama Ivan ambaye juzi alijifungua mtoto wake wa pili amesema hayo wakati akimshukuru wanamuziki Vanessa Mdee ‘Vee Money’ baada ya kumuona akimpigania mumewe kuhusu sanaa yake na kusema kuwa Roma amekuwa akipitia magumu lakini kinachomshangaza zaidi kwanini yote hayo yanamkuta yeye tu.
“Mungu akubariki wifi yangu, ahsante sana Vanessa Mdee, ila mume wangu anakutana na nyakati ngumu na changamoto sana kwenye muziki wake, hadi kuna wakati natamani uache muziki, ila najiuliza kwanini kila siku wewe tu? Haina tatizo endelea kupambana kwani hata hili litapita,” alisema Mke wa Roma Mkatoliki.
Manmo Aprili 5, mwaka jana, Roma na wenzake watatu walitekwa na watu wasiojulkana akiwa katika studio za Tongwe Records na kuonekana baadaye akiwa na majeraha mwilini mwake huku kidole chake kikiwa kimevunjwa.
Pia, makini Machi 1, 2018 Serikali kupitia Wizara ya Habari, Sanaa na Utamaduni ilimfungia msanii Roma Mkatoliki kutojihusisha na shughuli zozote za sanaa ya muziki kwa kipindi cha miezi sita kutokana na kukaidi kufanyia marekebisho wimbo wake wa ‘Kibamia’.